Na Paul Kasembo-TMC
MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewaagiza Wataalamu kusaidia katika utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya fedha wanazopatiwa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) ili waweze kuanzisha miradi itakatowaendeleza wenyewe.
Dkt Batilda aliota kauli hiyo wakati wa Kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF na kutoa mwongozo wa utambuzi na uandikishaji wa kaya za walengwa katika eneo la Utekelezaji kwenye Manispaa ya Tabora.
Alisema fedha wanazopata walengwa wanaweza kuzitumia katika shughuli mbalimbali ikiwemo ufugaji wa nyuki, kuku na mifugo mingine ambayo itawakomboa na kuwafanya wapande daraja na kuacha kutegemea ruzuku ya Serikali.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kupitia TASAF kaya zaidi milioni 1 zimenufaika na kufanyakazi za ujasiriamali na kuweza kuendesha maisha yao kwa unafuu ukilinganisha na awali.
Balozi Dkt. Batilda alisema Mkoa wa Tabora unazofursa nyingi kama vile mistu mikubwa , ardhi ya kutoa na mifugo mingi ambapo walengwa wanaweza nao kutumia nafasi hizo kusonga mbele kimaisha.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa aliagiza kufungwa kwa Kamera za ulinzi (CCTV Camera ) katika maeneo makubwa ya biashara ikiwemo minadani masokoni, na stendi ili kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali yaliyopo Tabora Manispaa.
Alisema sanjari na hilo ni vema Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ikaimarishwa ili kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Balozi Dkt. Batilda alisema katika maeneo ambayo yamefungwa mifumo ya TEHAMA imeonyesha mafanikio makubwa ambapo mapato ya Serikali yapanda mara tatu ya awali.
Awali Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) Emmanuel Macha alisema utambuzi wa awamu utafanywa kwa makini na wahusika watakula kiapo ili kuepuka kuingiza majina ya watu wasiostahi. Halmashauri ya Manispaa ya Tabora itapata nafasi ya kuibua na kuandiskisha walengwa wa Kaya Masikini sana wapya ambao hawakupa nafasi klwenye Tasaf iliyopita
Na MKUU wa Wilaya ya Tabora Dkt.Yahya Nawanda ambaye pia alihudhuria kikao hicho amesema hatasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa watu ambao hawana sifa ya kupokea fedha kwa ajili walengwa wa mpango wa kunusuru kaya Maskini (TASAF)
DC Dkt. Nawanda aliota kauli hiyo wakati wa Kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF na kutoa mwongozo wa utambuzi na uandikishaji wa kaya za walengwa katika eneo la Utekelezaji kwenye Manispaa ya Tabora.
Alisema fedha hizo zinatolewa na Serikali kwa ajili ya kuziwezesha Kaya Maskini ziweze kujikimu katika mahitaji muhimu ikiwemo upatikanaji wa huduma za chakula, elimu , afya ili ziliweze kushiriki vizuri katika shughuli nyingine za maendeleo.
Dkt. Nawanda aliwataka TASAF kushirikiana na Madiwani wa Manispaa ya Tabora wakati wa utambuzi na uandikishaji wa Kaya Maskini ili kuepuka kuwaacha walengwa.
Alisema kitendo cha kuwaacha walengwa kinaweza kusababisha lawama na malalamiko kwa Madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchi na wako karibu na wanatambua hali halisi za watu wao.
“Tumieni mbinu shirikishi kuwabaini walengwa ili malalamiko yalipo kwa baadhi ya kaya maskini yasiweze kujirudia tena” Dkt Nawanda alisisitiza.
Kwa upande wa Afisa Mfuatiliaji Manispaa ya Tabora Nisalile Mwaipasi alisema kwamba madiwani wanawajibu mkubwa kuhakikisha wanashirikina ili kuweze kutimiza lengo la serikali ya kutambua kaya masikini .
‘’sisi wote tunajenga nyumba moja hakuna haja ya kugombea fito jambo ambalo litarudisha nyumba malengo ya serikali ‘’alisema Mwaipasi.
Mwisho
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.