1.0 UTANGULIZI:
Chimbuko la Mji wa Tabora ulianzishwa katika nusu ya kwanza ya karne ya 19 na wafanyabiashara wa-Kiarabu na wa-Kiswahili kutoka Zanzibar. Waliutumia mji huu kama kituo cha njia ya biashara kati ya Pwani na Ziwa Tanganyika. Biashara kuu ilikuwa ni ya Pembe za Ndovu na Utumwa.
Mji wa Tabora ni moja ya miji inayokuwa kwa kasi katika Tanzania, Tabora ipo katikati ya ukanda wa Magharibi na hivyo kuufanya mji huu kuwa na uwezekano wa kuuza bidhaa zake katika Mikoa ya Kigoma, Rukwa, Singida, na Shinyanga, hivyo mji wa Tabora ni kitovu cha uchumi katika kanda ya Magharibi. Aidha kuwepo kwa station kubwa ya reli kutoka Mwanza, Kigoma, Mpanda na Dar es salaam ambayo iko sambamba na barabara zinazounganisha mji huu na Miji ya Kigoma, Mpanda, Dodoma, Shinyanga na Mbeya kunadhihirisha kuwa Tabora iliwekwa ili kuwa kitovu cha biashara katika Kanda ya Magharibi na kuwa kiunganishi kati ya Kanda ya juu kusini kunakolimwa mazao ya chakula kwa wingi na Kanda ya ziwa ukanda wa wafugaji.
Hata hivyo, Serikali ya Jamuhuri ya Mungano ya Tanzania imetambua umuhimu wa Mji wa Tabora, kwa kuwa tayari imeweka mipango yake mikubwa katika Mkoa kwa kuboresha miundombinu ya barabara na uwanja wa ndege pamoja na kukubali kuanzisha vyuo vya elimu ya juu na ya Kati, vitu vyote hivi vinaufanya mji wa Tabora kuwa ni sehemu bora ya kuwekeza katika ukanda huu wa Magharibi mwa Tanzania
Kuwepo kwa wawekezaji wa viwanda katika Mji wa Tabora kutaongeza ajira, kutakuza viwanda vidogo vya kusindika na kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa katika mkoa wa Tabora na Mikoa jirani. Aidha, kutakuza soko la mazao yanayozalishwa katika Vijiji vya Mkoa huu na hatimaye kupunguza umaskini uliokithiri.
2.0 FURSA ZILIZOPO KATIKA MJI WA TABORA
Mji wa Tabora ni Makao Makuu ya Mkoa wa Tabora na upo katikati ya Wilaya nyingine. Mkoa una zaidi ya mizinga milliom 3 ambayo inazalisha 50% ya asali yote inayozalishwa Tanzania, lakini hakuna kiwanda kikubwa cha kusinda asali na nta.
Kwa kuwa mji wa Tabora ni kitovu cha uchumi na biashara katika Mkoa kuna fursa kubwa ya kuwekeza viwanda vya kusindika asali na anta ili kuongeza thamani ya asali na kipato cha wafugaji. Kwa takwimu zilizopo Mkoa una uwezo wa kuzalisha tani 21,000 kwa mwaka.
Aidha, asali kutoka Tabora inauzwa Dar es salaam, Arusha na Nairobi ambako kuna viwanda na hivyo kuwakosesha wananchi wa Tabora ajira na kipato.
Mafuta ya alizeti na karanga ya napendwa sana na watumiaji kwa sababu hayana kiasi kikubwa cha chorestrol. Mji wa Tabora tunaagiza mafuta ya kula kwa asilimia 50% ya mahitaji kutoka katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Singida na Mwanza. Ambapo mahitaji yetu kwa mujibu wa takwimu kutoka Shirika la Chakula Duniani (FAO) kwa mwaka ni tani 15,000.
Aidha, Tabora ina ardhi nzuri ambayo inafaa kwa kuzalisha karanga na alizeti. Hivyo, kuna fursa kubwa ya kuwekeza kwenye kilimo cha alizeti na karanga na kuanzisha viwanda vya kusindika mafuta ya alizeti.
Tabora ni Mkoa wa tatu kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo , lakini cha kusikitisha kuna kiwanda kimoja cha kusindika maziwa ambacho kinafanya kazi chini ya uwezo wake. Hii inatokana na mitambo kuchoka, pia hakuna kiwanda cha kusindika nyama na ngozi inagawa vitu hivi vinahitajika kwa wingi.
Tabora ni mji wa kihistoria ambao umebahatika kuwa na vivutio vingi vya utalii lakini havijatangazwa ili kujua Tabora kuna vitu gani kama miji mingine. Vivutio hivi ni kama ugalla game reserve, kigozi game reserve, kituo cha makumbusho cha Dr. Livingstone –Kazehil, Kabuli la Mtemi Milambo, njia ya watumwa, hospitali ya kwanza Tanzania, Boma ambalo lina handaki linalounganisha Boma na Station. Vivutio hivi vinatoa fursa za kujenga hotel za kitalii pamoja na camping lodges.
Tabora ni mojawapo ya Mikoa mitano inayozalisha maembe kwa wingi, maembe yanasafirishwa kwenda Dar es salaam, mengi yanaharibika njiani, hivyo kuna umuhimu wa kuwa na kiwanda cha kusindika maembe katika mji wa Tabora.
Hata hivyo kwa kuwa Tabora ipo kwenye ukanda wa misitu ya miombo, kuna matunda mengi yanayozalishwa kwenye misitu ya miombo kama vile ntalali na ntonga ambayo yanatumika kutengenezea wine.
Mji wa Tabora ni miongoni mwa miji inayokua kwa kasi kubwa kutokana na kuwepo kwa taasisi mbalimbali. Kwa kipindi cha miaka michache iliyopita idadi ya watu imeongezeka kwa kasi kubwa ya 5% kwa mwaka (Census report, 2012). Sambamba na ongezeko hili la watu pia mahitaji ya vitu muhimu yameongezeka kwa kasi, lakini katika Mji wa Tabora hakuna supermarket kubwa/ shopping mall ambayo inaweza kuwa ni kimbilio la watu wengi. Hivyo kuna fursa kubwa ya kuwekeza supermarket ndani ya mji wa Tabora.
Mji wa Tabora ni moja ya miji inayokuwa kwa kasi katika Tanzania, Tabora ipo katikati ya ukanda wa Magharibi na hivyo kuufanya mji huu kuwa na uwezekano wa kuuza bidhaa zake katika Mikoa ya Kigoma, Rukwa, Singida, Shinyanga na nchi jirani za Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),Zambia na Malawi. Hivyo mji wa Tabora ni kitovu cha uchumi katika kanda ya Magharibi. Aidha kuwepo kwa station kubwa ya reli kutoka Mwanza, Kigoma, Mpanda na Dar es salaam ambayo iko sambamba na barabara zinazounganisha mji huu na Miji ya Kigoma, Mpanda, Dodoma, Shinyanga na Mbeya kunadhihirisha kuwa Tabora iliwekwa ili kuwa kitovu cha biashara katika Kanda ya Magharibi na kuwa kiunganishi kati ya Kanda ya juu kusini kunakolimwa mazao ya chakula kwa wingi na Kanda ya ziwa ukanda wa wafugaji.Kutokana na hali hiyo kuna mahitaji makubwa ya kuanzisha Bandari ya nchi Kavu na ukanda maalumu wa uwekezaji {Export Processing Zone (EPZ) na Special Economic Zone(SEZ)}
Eneo linalopendekezwa kwa ajili ya Bandari ya nchi Kavu, EPZ na SEZ lipo katika Kata ya Ndevelwa karibu na uwanja wa ndege kandokando ya reli ya kati itokayo Dar es Salaam na kuelekea mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Kigoma na Katavi. Katika eneo hili kutakuwa na eneo la uunganishaji (assembling) wa mitambo mbalimbali ya zana za Kilimo (Matrekta), magari na mashine zingine ili kuondokana na dhana ya Uchumi tegemezi
Ili kuboresha mazingira mazuri ya uwekezaji, pia tunahitaji kuboresha huduma za jamii. Kuna fursa ya kuwekeza katika sekta ya afya, mbali na Hospitali ya Mkoa hakuna hospitali nyingine ndani ya mji wa Tabora ambayo inaweza kuwa kimbilio kwa wawekezaji. Hata hivyo bado kuna fursa kubwa ya kuwekeza kwenye sekta ya elimu hasa katika vyuo vya ufundi na shule za sekondari yenye hadhi ya kimataifa ili kuvutia wawekezaji wakubwa.
Mji wa Tabora ni miongoni mwa miji mikongwe na na unakua kwa kasi kubwa kutokana na kuwepo kwa taasisi mbalimbali. Kwa kipindi cha miaka michache iliyopita idadi ya watu imeongezeka kwa kasi kubwa ya 5% kwa mwaka (Census report, 2012). Sambamba na ongezeko hili la watu pia mahitaji ya usafari wa daladala yameongezeka kwa kasi. Halmashauri ya Manispaa kwa kushirikiana na SUMATRA wameanzisha njia 12 kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri ndani ya Manispaa ya Tabora. Njia hizi zote hazina magari ya kutoa huduma ya usafiri, badala yake watu wanatumia baiskeli na pikipiki. Hivyo kuna soko kubwa la uhitaji wa usafiri wa daladala ndani ya mji wa Tabora.
Tabora ni Mkoa wa kwanza kwa uzalishaji wa zao la tumbaku Tanzania. Zao hili linachangia zaidi ya 50% ya pato la Mkoa. Tumbaku yote inayozalishwa Tabora inapelekwa Morogoro kusindikwa na hivyo kukosesha mapato na ajira kwa wananchi wa Tabora. Hivyo, katika Mji wa Tabora kuna fursa kubwa ya kuwekeza kiwanda cha kusindika tumbaku ili kuongeza thamani ya zao la tumbaku na kuongeza ajira. Eneo lililopendekezwa kujengwa kiwanda hiki ni nyuma ya milima ya Hardas kata ya Malolo lina ukubwa wa ekari 50.
Mji wa Tabora ni miongoni mwa miji inayokua kwa kasi kubwa kutokana na kuwepo kwa taasisi mbalimbali. Kwa kipindi cha miaka michache iliyopita idadi ya watu imeongezeka kwa kasi kubwa ya 5% kwa mwaka (Census report, 2012). Sambamba na ongezeko hili la watu pia mahitaji ya nyumba za makazi, biashara na taasisi mbalimbali yameongezeka kwa kasi. Hivyo kuna soko kubwa la uhitaji wa nyumba ndani ya mji wa Tabora.
3.0 MAENEO YALIYOTENGWA KWA AJILI YA UWEKEZAJI
Katika Manispaa ya Tabora kuna maeneo ya aina tatu ya uwekezaji ambayo ni:-
Maeneo ambayo yalitengwa kwa ajili ya viwanda tangu zamani, maeneo haya yapo katika eneo la Kiloleni. Katika eneo hili kuna viwanja ambavyo bado havijaendelezwa na pia kuna viwanda ambavyo mitambo yake ni mibovu. Wamiliki wa viwanda na viwanja hivi wapo tayari kwa kuingia ubia na wawekezaji wengine. Mfano Tabora Misitu na Tabora Dairies. Eneo hili lina miundombinu yote (umeme, maji, Barabara na reli)
Maeneo mapya yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na hoteli.
Katika Manispaa ya Tabora maeneo haya yametengwa katika sehemu zifuatazo:
Eneo hili limeandaliwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya kati, lina jumla ya viwanja 40 vya wastani wa ekari 3 kwa kila kiwanja. Katika eneo hili kuna miundombinu ya barabara kuu, Reli na umeme.
Katika eneo hili upimaji bado haujafanyika kwa sababu fidia kwa wananchi wenye mashamba ya asili bado haijatolewa.
Aidha, katika eneo hili tayari kuna mwekezaji mmoja (MIHAN GAS LTD) ambae aligharimia fidia na akapimiwa viwanja na ameshaanza ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gas.
Katika eneo hili limepangwa kwa ajili ya viwanda vya kawaida (Light Industry) na lina ukubwa wa ekari 200, kwa ajili ya kuchakata mazao ya kilimo na mifugo. Katika eneo hili kuna reli na barabara.
Eneo hili bado halijapimwa kwa sababu fidia bado haijatolewa kwa wananchi wenye mashamba ya asili.
Katika eneo hili kuna fursa ya kujenga majengo ya vitega uchumi mfano ofisi, shopping malls, hotel, kwa kushirikiana na wamiliki wa viwanja na majengo yalipo katika eneo hilo. Eneo la mjini kati linaundwa na Kata nne ambazo ni Kanyenye, Chemchem, Gongoni na sehemu ya Kata ya Mbugani.
Hii ni kwa sababu katika eneo hili linatakiwa kujengwa ghorofa 4- 6 ambayo ni fursa kwa taasisi kubwa za uendelezaji majengo kama vile NHC, PSPF, TBA na LAPF. Aidha, Halmashauri kupitia kongamano la uwekezaji katika Mkoa wa Tabora, wananchi wenye viwanja katika eneo la Mjini kati tayari wameshaelimishwa na wapo tayari kuingia ubia na wawekezaji.
Aidha, Manispaa ya Tabora imeainisha eneo linguine kandokando ya Barabara kuu ya Itigi kwa ajili ya kujenga mji wa kisasa wa kibiashara lenye ukubwa wa ekari 100 katika eneo la Inala
.
MAENEO YALIYOTENGWA KWA AJILI YA UWEKEZAJI
No.
|
ENEO LILILOTENGWA
|
UKUBWA
|
MIUNDOMBINU
|
HALI HALISI
|
1.
|
Eneo la viwanda Malolo
|
Ekari 120
|
Umeme, barabara na reli
|
Eneo halijalipwa fidia na kupimwa
|
2.
|
Eneo la Viwanda Cheyo
|
Ekari 200
|
Barabara na reli
|
Eneo halijalipwa fidia na kupimwa
|
3.
|
Eneo la Viwanda Kiloleni
|
|
Maji, Umeme, Barabara na reli
|
Eneo limepimwa na linamilikiwa na wananchi ambao wapo tayari kuingia ubia na mwekezaji
|
4.
|
Eneo la Bandari ya Nchi kavu (Dry Port) na EPZA
|
Ekari 400
|
Barabara, reli, Umeme na Uwanja wa ndege
|
Eneo halijalipwa fidia na kupimwa
|
5.
|
Eneo la Mjini Kati – Mji mkongwe – (Central Business District)
|
Kata ya Kanyenye, Gongoni na Chemchem
|
Barabara, Maji, Umeme, na simu
|
Eneo limepimwa kwa matumizi ya biashara na Taasisi na linamilikiwa na wananchi wako tayari kuingia ubia na wawekezaji
|
6.
|
Eneo la Kilimo Mjini (urban agriculture) Ndevelwa
|
Hekta 131
|
barabara
|
Eneo halijalipwa fidia na kupimwa
|
7.
|
Eneo kwa ajili ya Hotel za kisasa – Mawiti na Kidatu na Itetemia
|
Hekta 25
|
barabara
|
Eneo halijalipwa fidia na kupimwa
|
|
|
|
|
|
8.
|
Maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Viwanda vidogo vidogo/Informal Sector
|
|
Ipuli Block D
Ipuli Block F Usule Block C Mawiti Block A |
Maeneo haya yamepimwa.
|
4.0 HATUA ZINAZOFANYWA NA SERIKALI KUVUTIA WAWEKEZAJI TABORA.
Halmashauri kwa kushirikiana na Serikali kuu imefanya jitihada zifuatazo ili kuboresha mazingira ya uwekezaji Tabora kama ifuatavyo:-
Kukamilisha ujenzi wa barabara za lami zinazounganisha Mji wa Tabora na Mikoa jirani
Kukamilisha ujenzi wa uwanja wa ndege
Umbembuzi yakinifu na Usanifu wa kina unaendelea ili kufikisha maji ya ziwa Victoria Mkoani Tabora.
Ukarabati wa mfumo wa maji ya bomba wa zamani ili kuongeza uzalishaji wake.
Kuweka mkongo wa Taifa wa mawasiliano ili kurahizisha mtandao wa mawasiliano
Kuandaa Mwongozo wa uwekezaji katika Mkoa wa Tabora na umekamilika
Kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo kupitia kongamano la uwekezaji ambalo lilifanyika Dar es salaam tarehe 19/07/2013 na kufuatiwa na kongamano la uwekezaji (Economic Forum) la tarehe 19/08/2015 ambalo lilifanyika Tabora.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.