Na Alex Siriyako,
Wataalamu ambao ni Wakuu wa Vitengo na Sehemu katika Manispaa ya Tabora wamepata Mafunzo ya Mwongozo wa Mfumo wa Taarifa za Kijiografia (GIS) leo Julai 10, 2023 katika Ukumbi wa Manispaa ya Tabora.
Mafunzo haya yametolewa na Mtaalamu kutoka Ofisi ya Rais-(TAMISEMI) Ndugu George Joseph Miringay ambae ni Afisa Mipangomiji Mwandamizi akiwa ameambatana na Eng. Rashid S. Jellan kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na ameeleza kuwa Mwongozo huu umeanza kutumika kuanzia Juni 2023.
GIS (Geographical Information System) ni mfumo wa taarifa za kijiografia ambazo hukusanywa kutoka kwenye Ramani za msingi na uwandani, huchakatwa na kuonyeshwa kwa kutumia Ramani za aina mbali mbali.
Mfumo wa taarifa za kijiografia (GIS) unatumika katika shughuli mbalimbali za uhandisi, mipango, usimamizi wa ardhi, usafiri na usafirishaji, shughuli za kuhesabu watu na makazi au mifugo, mawasiliano ya simu, biashara na kadhalika.
Ndugu George ameongeza kuwa, umuhimu mkubwa sana wa Mfumu huu wa GIS ni pamoja na Kuhimiza na kuimarisha matumizi ya takwimu za kijiografia (spatial data) kutumika kikamilifu katika kusaidia utoaji sahihi wa maamuzi, lakini vilevile na kuendeleza matumizi ya GIS kupitia miradi iliyotangulia (TSCP, ULGSP, DMDP, TACTIC)
Ndugu George amefafanua zaidi kuwa, Mwongozo unalenga kuwezesha Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuweka msisitizo unaohitajika na mikakati ya kuhimiza matumizi ya GIS kwenye ofisi stahiki ili kuimarisha utoaji maamuzi sahihi na kwa haraka katika kutoa huduma kwa wananchi na kuendana na mabadiliko ya teknolojia.
Mwezeshaji wa mafunzo amefafanua kuwa Halmashauri itaweza kuendesha na kutekeleza mfumo kwa kufanya yafuatayo;
Kuunda Timu za GIS, kujenga uwezo wa vifaa na wataalam, kuanzisha kanzi data za GIS kwa kila Idara na Vitengo, kuweka mikakati ya miaka 3 ya kuimarisha GIS, kushirikisha wadau wote kwenye utekelezaji, ikiwemo sekta binafsi na kuingia nao ubia wa kubadilisha takwimu, Kutenga ofisi maalum kwa ajili ya shughuli za GIS, Kutenga fedha kwenye bajeti zao kwa ajili ya kazi za GIS, pamoja na kuwasilisha takwimu na taarifa ya utekelezaji wa kazi za GIS katika Menejimenti, Mkoa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Kuhusu mpango kabambe (Master Plan) wa Halmashauri ya Manispaaya Tabora, mwezeshaji alisisitiza juu ya umuhimu wa uzingatiaji wa mpango kabambeuliopo katika uendelezaji wa ardhi unaofanyika ndani ya Manispaa na piaalishauri juu ya suala la elimu kuendelea kutolewa kwa wadau wote wanaohusikaatika utekelezaji wa mpango kabambe uliopo wa Mwaka 2015 – 2035.
Katika kuhitimisha mafunzo haya, mwezeshaji amesisitiza kuwakutakuwa na ufanisi katika utekelezaji wa Mfumo wa Taarifa za Kijografia (GIS) ikiwa kila mdau wa mfumo huu kuanzia TAMISEMI, MKOA, HALMASHAURI, KATA, MITAA,VIJIJI na WADAU WENGINE watashirikishwa na kushirikiana kwa kupeana taarifa zamsingi katika kila hatua ya utekelezaji.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.