Na Alex Siriyako:
Rai hii imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango leo Juni 6,wakati akifungua rasmi michezo ya UMITASHUMITA na UMISSETA Kitaifa inayofanyika hapa Mkoani Tabora, Manispaa ya Tabora.
Dkt. Mpango ameeleza kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kuboresha miundombinu ya Michezo Nchini hususani Mashuleni ambapo hadi kufika sasa shule 56 za Serikali zitatumika kama vituo vya michezo.
Aidha Mhe. Mpango ameagiza Wizara ya TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu wahakikishe kuwa kila shule ya Sekondari na Msingi inakuwa na angalau mwalimu mmoja wa michezo.
Vilevile Mhe.Mpango ameelekeza kuwa kila shule irudishe utaratibu wa Bras Bandi, ratiba ya michezo mashuleni izingatiwe, pamoja na kupanda miti ya kutosha kuzunguka viunga vya shule.
Mhe.Mpango amewaelekeza Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni kushirikiana na Wadau wengine wa michezo Nchini kukuza vipaji na washirikiane vilevile na Wizara ya Mambo ya Nje kutafuta fursa za Michezo nje ya Nchi.
Dkt.Mpango amehitimisha hotuba yake kwa kuwashukuru Wananchi wa Tabora kwa upendo wao mkubwa na kwa mapokezi yao mazuri kwake binafsi na kwa vijana wanaoendelea na michezo hii katika viwanja vya Tabora Boys na Tabora Girls.
Mwisho
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.