Na Alex Siriyako;
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Dkt. Peter Nyanja amewasainisha Mikataba ya Mpango wa utekelezaji wa shughuli za uboreshaji na usimamizi wa elimu kwa mwaka 2023. Tukio hili limefanyika leo tarehe 20 Januari, 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Tabora uliopo Makao makuu ya Halmashauri.
Mikataba hii kwa Waratibu Elimu Kata inafuatia maagizo ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambapo Maafisa Elimu ngazi ya Mkoa waliingia Mkataba na Wizara hiyo, mkataba unaowataka wapate matokeo chanya katika mitihani ya ngazi mbalimbali katika mikoa yao.
Vilevile Maafisa hawa wa ngazi ya Mkoa wanapaswa kuingia mikataba na Maafisa elimu ngazi ya wilaya kwaajili ya kupata matokeo hayo. Halikadhalika Wakurugenzi wa Halmashauri wameingia Mikataba hiyohiyo na Waratibu Elimu Kata ambao nao wameingia mikataba hiyo na Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu wa Shule.
Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu wa shule nao wataingia Mikataba hiyohiyo na Walimu wa masomo ambao ndio watekelezaji wa zoezi zima la ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi madarasani.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Dkt. Peter M. Nyanja amewasisitiza Waratibu wakafanye kazi na wahakikishe vigezo vyote 23 vya upimaji na utendaji kazi katika mkataba huo vinatiliwa mkazo.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.