Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora wameisisitiza Menejimenti ya Manispaa ya Tabora kuhakikisha kuwa wanatekeleza miradi ya maendeleo iliyowekwa kwenye Halmashauri ili iweze kuongeza mapato ya Halmashauri.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa robo ya kwanza Julai -Septemba kwa mwaka wa fedha 2019/ 2020 waheshimiwa Madiwani walisema ya kwamba, kumekuwa na utekelezaji wa kusua sua kwenye miradi ya maendeleo hasa ambayo inalengo la kuongeza mapato ya Halmashauri. Jmabo ambalo halikubaliki na kwamba halina afya kwa mustakabali wa mapato ya Halamashauri kwa ujumla.
Sambamba na hilo, baraza pia lilisisitiza ya kwamba Menejimenti iwe inapkea, zingatia na kutekeleza maelekzo na maagizo yote yanayotolewa ili kuepuka kurudia rudia jambo mara kwa mara kwakuwa hali hiyo inawafanya Waheshimiwa madiwani kukosa imani na Menejimenti kwakuwa kila wanachokuwa wanaagiza na kukubaliana hakitekelezwi kwa wakati unaotakiwa.
Katika mkutano huo wa tarehe 12-13/11/2019 ambao pia ulihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini Komanya Kitwala, pamoja na baadhi ya waalikwa wengine akiwemo Meneja TARURA Manispaa ya Tabora Mhandisi Edwin Kabwoto, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Tabora Mhandisi Seraphine Lyimo, Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Tabora Mabusi Peter wao pia walipata nafasi ya kuelezea kazi zao na mwisho Mkuu wa Wilaya ya Tabora aliongea na baraza la madiwani.
Akiongea kwenye wakati wa mkutano huo wa baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala aliwataka watumishi wa Manispaa ya Tabora kuwa waadlifu, watangulize uzalendo kwanza kwenye kazi zao za kila siku ili waisaidie Serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.
‘’Kumekuwa na sabotage(hujuma) kwa baadhi ya watumishi wasiokuwa waaminifu wa Manispaa ya Tabora ambao wamekuwa wakihujumu juhudi zote zinazofanywa kwa ajili ya kuiletea maendeleo Manispaa, nakuagiza Mkurugenzi wa Manispaa kuhakikisha unakaa na Menejimenti yako yote na kuwaita wale wote wanaosemwa semwa vibaya uzngumze nao na wale wasiostahili uwaondoe kwnye maeneo hayo wanayo lalamikiwa ili wawekwe wengine, alisema Komanya.’’
Komanya alitumia fulsa hiyo pia kumtaka Meneja wa TARURA Manispaa ya Tabora kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi wa Manispaa ya Tabora juu ya matumizi sahihi ya barabara hizi za mijini kwakuwa wengi wao hawana uelewa sahihi juu ya namna ya kuzitumia. Pia akamtaka kuwepo na namna nzuri ya ukusanyaji wa mapato yao hasa yale yanayotokana na faini za kuegeshaji mbaya wa gari katikati ya mji, na kuwe na faini ya kufanana siyo mwananchi mwingine atozwe 20,000/ na mwingine atozwe 50,000/ wakati kosa ni la kufanana.
Na kwamba atapaswa kuwa anahudhuria mikutano ya baraza la madiwani kwa ajili ya kwenda kusoma mpango kazi wake wa kila robo ya mwaka. Katika maelekezo yake pia kwa upande wa Waheshimiwa Mdiwani aliwataka kuwa kitu kimoja na kutanguliza uzalendo na maslahi mapana hasa ya linapokuwa limetokea suala linalohusu Manispaa ya Tabora.
Awali kwa siku ya kwanza Baraza la Madiwani lilipokea na kujadili taarifa mbali mbali za robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2019/2020 zikiwemo za utekelezaji wa Julai – Septemba 2019/2020, ambapo siku ya pili baraza lilipokea na kujadili taarifa mbali mbali za utekelezaji kwa Julai – Septemba 2019/2020 kutoka kwenye Kamati za kudumu za Waheshimiwa Madiwani.
Pamoja na mambo mengine mazuri yanayofanywa na Hamlashauri ya Manispaa ya Tabora, lakini pia Menejimenti iliweza kuibua miradi kadhaa ikiwemo ya ujenzi wa vyumba 24 vya maduka eneo la stendi ya basi, kuweka geti kwenye eneo la kuingilia na kutoka kwa gari ndani ya stendi ya basi, soko jipya la kuteremshia matunda, mazao na mizigo ya jumla eneo la Tambukareli, eneo la kuuzia mbao, furnitures (samani kama vile sofa n.k) ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuongeza mapato kwa Manispaa ya Tabora.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.