Wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora sasa kuanza kunufaika na vifurushi vya Mfuko wa Afya ya Jamii ulioborehwa. Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggey Mwanri alipokuwa akiongea leo Ofisini kwake na waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali.
Mwanri alimeeleza ya kwamba kwa sasa Serikali ya awamu ya tano imekuja na mpango mkakati mzuri wa kuwezesha na kuhakikisha kuwa wananchi wake wanapata huduma ya matibabu kwa gharama nafuu kabisa kupitia Mfukowa Afya ya Jamii ulioboreshwa, yaani CHF ILIYOBORESHWA.
“Katika mkakati huo kila kaya yenye jumla ya watu sita (6) watapatiwa huduma ya matibabu kwa mwaka mzima kwa gharama ya Tzs 30,000/ tu nah ii twaweza kuiita ni MAGUFULI CARE kama ilivyokuwa ile ya OBAMA CARE maana inalenga kuokoa uhai wa wananchi waliowengi wenye kipato cha chini”, alisema Mwanri.
Aidha kupitia kikao hicho Mwanri alitangaza MICHANGO YA VIFURUSHI VYA NAJALI AFYA, WEKEZA AFYA, NA TIMIZA AFYA ambapo vinalenga kuleta unafuu mkubwa kwa wananchi kupata huduma ya matibabu kwa gharama ndogo na mgonjwa atatibiwa sehemu yoyote ile hapa nchini.
Sambamba na hayo Mwanri alitumia fulsa hiyo kuwaelezea waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa kama ifuatavyo;
>Upanuzi wa wigo wa huduma ya CHF, ambapo alisema kupitia mpango huu wa CHF ILIYOBORESHWA serikali imejipanga kupanua wigo kuwa mkubwa zaidi ili walengwa waweze kupata huduma za matibabu kwenye vituo vyote vya serikali ambapo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kuna jumla ya vituo 23.
>Huduma za CHF zitatolewa kuanzia, katika utoaji wa huduma hizi walengwa wanaweza kupata tiba kuanzia ngazi ya Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali za Wilaya hadi Hospitali za Mikoa kwa utaratibu mzuri wa rufaa uliowekwa.
>Gharama za kujiunga, kwa upande wa gharama za kujiunga na huduma hii itakuwa ni Tzs 30,000/= kwa kaya yenye jumla ya wanufaika sita (6) itakayolipwa kwa mkupuo na kupata huduma kwa mwaka mzima.
>Upatiakanaji wa dawa, walengwa wote wataweza kupata dawa kwenye vituo vyote na kwamba dawa zipo za kutosha.
>Usajili wa wanachama, zoezi la usajili wa wanachama litafanywa na waandikishaji waliochaguliwa katika ngazi zote za Mitaa na Vijiji na kadi atapatiwa papo hapo kwakuwa kazi hiyo inafanywa kwa simu ambazo zimeunganishwa moja kwa moja kwenye mfumo.
Aidha Mwanri alibainisha ya kwamba, mwanachama hatahitajika kubadilisha kitambulisho chake baada ya muda wa mwaka mmoja kuisha, badala yake atahitajika kulipia Tzs 30,000/= na kisha kuendelea kunufaika na huduma kwa mwaka unaofuata.
Kwa upande wake Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii Mkoa wa Tabora Baraka Mahona akisema ya kwamba katika utekelezaji wa mpango huu, wameanza na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora. Ambapo mpaka sasa hivi kuna jumla ya waandikishaji 175, vituo vya kuandikishia na kutoa huduma vipatavyo 23.
Programu ya CHF ILIYOBORESHWA ilizinduliwa rasmi hapa Tabora tarehe 25 Januari, 2019 na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ikiwa na lengo la kumrahisishia mwananchi mweneye kipato cha chini kuweza kuwa na uhakika wa kupata huduma ya matibabu wakati wote pamoja na wategemezi wake wapatao sita (6) kwa gharama hiyo hiyo ya Tzs 30,000/=
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.