Na Paul Kasembo-Shinyanga.
Ziara ya siku mbili kwa Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Tabora imekamilika leo katika Halmasahuri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kutembea na kuiifunza katika shuguri za uendeshaji wa miradi midogo na ya kati iliyopo katika eneo la Viwandani, uanzishwaji na utunzaji wa dampo lililopo Kazimzumbi Kilomita 6 kutoka Mjini kati, uanzishwaji na uendeshwaji wa machinjio ya kisasa Ndembezi ilyopo Kilomita 5 kutoka Mjini kati.
Akitoa salamu na ujumbe kutoka Manispaa ya Tabora, kaimu Mkurugenzi wan dg Gudu Malulu aliwaeleza wenyeji kuwa lengo la kusafiri kwenda Shinyanga ni kujifunza namna ambavyo wamefanikiwa mambo mbalimbali ka,a yalivyotajwa hapo juu.
”Kwa dhati kabisa tumedhamiria kuja kujiunza na kuchukua yale yote yenye tija kubwa yatokanayo na ziara hii ili yaende kuwa msaada mkubwa kwa Mnaispaa yetu ya Tabora kwa muktadha wa kuipaisha Kiuchumi, kuboresha huduma za jamii, kuongeza na kuimarisha mapato na kimaendel;eo kwa ujumla ili kufikia malengo ambayo Manispaa imejiwekea hasa kwa kip9ndi cha mwaka wa fedha 2022/2023”, alisema Malulu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Ndg Jomaary Satura alisema kuwa ni faraja sana kwa Wana Shinyanga kwa kutembelewa na ugeni kama huo muhimu ja bora zaidi wenye lengo la kuja kujifunza mambo ambayo wameyaona ni mema kwao na yanapatika katika Manispaa ya Sahinyana, na kwamba aliwaahidi ushirikiano wa kutosha zaidi ili waridhike na wapate walichokusudia na kiende kuwa na ,matokeo chanya kwa wananchi wao.
Satura alisema kwamba Shinyanga siyo bora zaidi kukiko Halmashauri zingine, lakini kitendo cha Manispaa ya Tabora kuichagua Shinyanga ni jambo jema na lenye kuketa faraja kubwa sana, na kwamba Manispaa ya Shinyanga itakwenda kujinza pia mambo mazuri kutoka Manispaa ya Tabora.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe Elias Masumbuko, aliwashukuru sana Waheshimiwa Madiwani Kutoka Manispaa ya Tabora kwa kuiona Shinyanga na hata wakaamua kwenda kujifunza, hivyo akawaomba kuwa huru kuuliza, kuhoji, kukosoa na kuboresha pale ambapo wanaona panafaa kwa kusudoo la kuleta tija na kuwahudumia wananchi wa Manispaa ya Shinyanga.
“Siyo kwamba tuu mmekuja kujifunza kutoka kwetu, hapana nasi pia kupitia ujio wenu tutajifunza mambo mengi yaliyomazuri zaidi ambayo mmekuja nayio na huenda sisis hatukuwa nayo pia, ndiyo maana nasema mkosoe, mshauri na mhojinkwa kadiri mtavyoona ili nasi tujikosoe pia,” alisema Meya Masumbuko.
Akifunga ziara hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora, Mhe. Ramadhani Kapela aliwashukuru sana wanaShinyanga kwa ukarimu wao waliowapatia tangu kufika kwao hapo, ushirikiano waliowaptaia kwenye ziara hiyo ya kujifunza mambo mbalimbali na kwamba akwaahidi wajumbe wote kuwa watakwenda kuyafanyia kazi yote yale waliyojifunza ili yakalete mabadiliko chanya zaidi kwa wananchi wa Manispaa ya Tabora.
Kukamilika kwa ziara hiyo ya siku mbili katika Manispaa ya Shinyanga, kunatoa fulsa sasa kwa wao Waheshimiwa Madiwani kwenda kuyachakata na kuyabadilisha yale yote waliyojifunza na kuyaona kwenye ziara hiyo ili yakaonekane kwenye madiliko ya vitendo na maisha ya wananchi wao wanaowaongoza kwenye maeneo yao, sambamba na kukuza pato la Manispaa, kuboresha huduma kwa jamii, kuibua na kusimamia mairadi yao wenyewe.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.