KAMATI ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa imeiagiza Halamshauri ya Manispaa ya Tabora kuhakikisha ndani ya mwezi huu wanajenga vibanda katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendeyo mikoani kwaajili ya abiria kupumzikia wakati wakisubiri usafiri.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa Jasson Rweikiza wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo walipotembelea vyanzo mbalimbali ilikujionea hali ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Alisema hali iliyopo sasa sio nzuri na inawasababishia adha wasafiri na kuongeza kuwa vibanda hivyo vitasaidiakuwaondolea wasafiri adha ya kupigwa jua na kunyeshewa mvua wakati wanawasilikutoka maeneo mbalimbali au wakati wakisubiri usafiri.
“Ndugu zangu mumeona hata sisi imebiditutafute mti ndio kufanyie kikao chetu hiki…ni lazima mjenge sehemu ya abiria kukaa na kujikinga kama wakati wa mvua au jua kali…msiwaache wasafiri waendeleekuteseka” alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa ni vema Halmashauri iongeze nguvu katika ukusanyaji wa mapato kutokana na vyanzo mbalimbali vilivyopo katika Stendi hiyo.
Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Rombo Joseph Selasini aliutaka uongozi wa Stendi hiyo kuhakikisha Mawakala wa Mabasi hawawabughuzi wasafiri wanaohitaji kusafiri .
Naye Naibu Waziri wa Nchi Ofisi yaRais TAMISEMI, Josephat Kandege aliitaka Halmashauri ya Manispaa hiyo kuhakikisha wanasimamia vizuri ukusanyaji wa mapato katika huduma mbalimbali ikiwemo vyoo ambapo alisema mapato ya shilingi 700,000/- kwa wiki kwa huduma ya choo ni kidogo ukilinganisha na idadi ya watu wanaotumia stendi ya Tabora.
Aliwataka watendaji kujifunza kutoka Halmashauri ya Mji Nzega ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato katika huduma ya choo katika stendi yao.
Mwisho
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.