Ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yamefanyika leo katika viwanja vya Fatuma Mwasa (nane-nane) vilivyopo Kata ya Ipuli, Manispaa ya Tabora Mkoani Tabora ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde (MB).
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mhe Mavunde alisema kwamba Ushirika ni nyenzo muhimu sana kwa muktadah wa wana ushirika wenyewe, jamii na Taifa kwa ujumla. Kwakuwa ushirika una tija kubwa sana kwani kwa mwaka ujao wa fedha 2022/2023 Serikali imejipanga Zaidi kuimarisha Kilimo kwa kuanza na kutoa pembejeo zote ikiwamo mbolea, mbegu nk.
Ambapo kufikia mwaka 2030 Sekta ya kilimo itakuwa imekua kwa asilimia kumi na hayo ndiyo maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Mavunde aliwaeleza wana ushirika kuwa Serikali kwa mwaka wa fedha ujao imeongeza bajeti yake kutoka Tzs Bilioni 294 hadi 954, kwenye umwagiliaji imeongeza kutoaka Bilioni 46 hadi 361 ambapo itaimarisha Zaidi mabonde 22 yakiwamo Manonga, Pangani, Maragalasi, nk. Yote hayo yatafikiwa.
Yote hayo yanafanyika ili kuwaondelea wakulima dhana ya kilimo cha kutegemea mvua za msimu pekee na badala yake wawe na kilimo endelevu wakati wote ambapo sasa Serikali itajenga mabwawa 12, Skimu za Umwagiliaji 48 zitakarabatiwa kwa mwaka 2022/2023.
“Tunamtaka mkulima wa Tanzania kuacha kutegemea kilimo cha mvua za msimu na badala yake aanze kuwa analima wakati wote, kwa kufanya hivyo kutaweza kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, vikundi, kupunguza umasikini na kuongeza ajira kwa Taifa,” alisisitiza Mhe. Mavunde.
Aidha Mhe. Mavunde amesema kuwa Serikali inatarajia kuanza kugawa mashamba kwa vijana ikiwa ni sehemu ya kuongeza ajira ambapo mashamba hayo yatafyekwa, kuandaliwa nan a kukabidhiwa kwa vijana hao ambapo pia watapatiwa pembejeo zote muhimu na vitendea kazi, na kwa kuanzia wataanza na Mkoa wa Dodoma kwa majaribio ambapo kutakuwa na Hekari 20.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Tabora ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Yahaya Esmail Nawanda, alimueleza mgeni rasmi pamoja na wananchi waliokuwa wamehudhuria hafla hiyo kuwa, Mkoa wa Tabora unayo furaha kubwa sana kuteuliwa kuandaa maadhimisho hayo ya Siku ya Ushirika Duniani, na kwamba unamshukura sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yeye Naibu Waziri kwa kuitia ombi la kufika na kufungua maonesho hayo.
Mhe. Nawanda alimueleza kuwa kwa Mkoa wa Tabora wamefanikiwa kurjesha Chama Cha Ushirika Manonga kilichopo Wilaya ya Igunga tangu tarehe 13/6/2022 ambacho sasa kitarejesha tena uzalishaji wa Pamba eneo hilo, jambo ambalo lilikuwa likiwezesha kuongeza jaira kubwa na kukuza uchumi pia.
N kwamba Mkoa wa Tabora unatambua na kuthamini sana mchango mkubwa wa Ushirika katika maeneo yote, kwakuwa imekuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi na Taifa kwa ujumla, huku akiwataka wananchi wa Mkoa wa Tabora kwenda kutembelea maonesho hayo na kujifunza vitu vingi Zaidi vinavyofanyika katika viwanja hivyo.
Maonesho hayo ya Siku ya Ushirika Duniani yamefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 28/6/2022 na yanatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 2/7/2022. Ambapo kwa mwaka huu maonesho yaliongzwa na Kauli Mbiu; USHIRIKA HUJENGA ULIMWENGU BORA.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.