Na. Paul Kasembo.
Wakazi wa Wilaya ya Tabora wamekumbushwa kutambua na kuthamini thamani yao kubwa waliyonayo juu ya harakati za kuiletea Uhuru Tanzania kuwa uhuru wa Tanganyika uliasisiwa Mkoani Tabora kufuatia kura Tatu za Uwamuzi wa Busara kuhusu kupatikana kwa Uhuru wa Nchi zilizopigwa zikiratibiwa na hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambapo wanatakiwa kuuthamini na kuupa hadhi inayostahili ikiwa na wao wenyewe kujithamini kwakuwa wanamchango mkubwa.
Hayo yalibainika katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika Kimkoa yaliyofanyika katika uwanja wa Chipukizi ambapo jamii ilihimizwa kutambua kuwa Uhuru sio wa Tanzania bali ni wa Tanganyika.
Akitoa hutuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa waTabora Balozi Dk. Batrida Burian, Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Louis Bura alisema kuwa Mkoa huo ndiyo chimbuko la Uhuru wa Tanganyika na kwamba Mkoa huo umeasisi mambo mengi makubwa katika Nchi hii ikiwa katika Sekta ya Elimu, Afya, Miundombinu, Uwezashejai wananchi kiuchumi ambapo kuna asilimia 10 za wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu, KIlimo, uwekezaji na kuwa Nchi ya Viwanda.
“Unajua kuna watu wanajua ni Uhuru wa Tanzania Bara, hapana ni wa Tanganyika na ulipatikana hapa mjini Tabora Mkoani huu wa Tabora na baada ya kufanyika Uamauzi wa Busara kwa kupigwa Kura Tatu kuamua kujipatia Uhuru wetu chini ya Baba yetu wa Taifa hayati Mwl. Nyerere,” alisema Mhe. Bura.
Ukitazama Katika mwaka 2021/2022 mbegu zilizosambazwa ni asilimia 14.7, maji yamesambazwa asilimia 75 Mijini na asilimia 57.9 Vijijini na mapato ya ndani tulipata Zaidi ya Tzs Bilioni 5.8 yote hayo ni matunda ya uhuru, kwa kifupi Wilaya Tabora imetoa vingozi wenye wadhifa mkubwa sana hapa akiwemo Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere.
Alisema kuwa kulikuwa na changamoto katika Sekta ya barabara, maji, nishati na nyingine ambazo Serikali imezifanyia kazi ili kuzimaliza nakuhakikisha maendeleo ya uhakika yanapatikana ili kazi ya kuwahudumia wanachi iendelee daima.
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Dr. Peter Maiga Nyanja alitoa taarifa kuwa katika maadhimisho hayo mapema asubuhi walipanda miche ya miti 8,000 kati yake 3,000 waliipanda Brigedia ya Tabora na 5,000 katika maeneo mengine ya Mjini na katika Taasisi mbalimbali.
Dk.Nyanja alisema kuwa walikwenda kutoa huduma ya matendo ya huruma katika kambi ya wazee kwenye Kata ya Mpela, kituo cha kulelea watu wasiojiweza cha Charitas kilichopo Jimbo Kuu Katoriki, usafi katika Hospitali ya Rufaa Kitete na kuwapatia pesa taslimu ikiwa ni gharama ya Zaidi ya pesa taslimu jumla Tsh. milioni 5.
Pamoja na yote hayo, pia maadhimisho yalipambwa na michezo mbalimbali ikiwamo riadfha, kongamano nk.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Manispaa Tabora, 4 Barabara ya Kiwanja cha Ndege
Anwani ya Posta: S.L.P 174, 45182 Tabora
Simu ya Ofisi: +255 262606088
Simu ya Mkononi: +255
Barua Pepe: md@taboramc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.