Mkuu wa Mkoa wa Tabora MHE. DKT PHILEMON SENGATI anatarajiwa kuzindua kitabu cha mwongozo wa wa uwekezaji wa Mkoa wa Tabora tarehe 8 Mei. 2021 hafla ambayo itafanyika kwenye ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo Mgeni rasmi wa tukio atakuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geofrey Mwambe (MB).
Hayo ameyasema leo kwenye kikao na waandishi wa habari ambapo alikuwa akitoa taarifa kwa umma juu ya uwepo wa tukio hilo muhimu lenye muktadha wa uchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla ili umma uweze kuelewa na kufuatilia tukio hilo hata kwa kupitia vyombo vya habari.
”Kwa kuwa ninyi ni wadau muhimu sana wa maendeleo katika Mkoa wetu, nimeona ni vema niwaite hapa ili niwafahamishe kuhusu tukio hilo muhimu kwa uchu,I wa Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla ili nanyi kwa kutumia taaluma yenu mtangaze na kuhamasisha wananchi wa Mkoa wa Tabora, na Watanzania wote kufuatilia kwa karibu tukio hilo katika vyombo vya habari,’’ alisema Dkt Sengati.
Dkt Sengati alisema kuwa, umuhimu wa Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Tabora unaelezea fulsa muhimu zilizopo Tabora ili sasa kumrahisishia mwekezaji kufanya maamuzi ya kuwekeza Tabora. Pia itaweza kumsaidia mwananchi kufahamu jinsi ya kunufaika na uwekezaji tarajiwa.
Kwenye kitabu hicho kumeainisha maeneo muhimu ya kiuwekezaji ikiwa ni pamoja na;
Aidha Sengati alikumbusha kwamba, mnamo tarehe 01 Julai, 2020 Tanzania iliingia katika uchumi wa kati ambao msingi wake mkuu ni viwanda , hivyo akawaomba wananchi wote wa ndani na nje yaTanzania kuchangamkia fursa hii ili waweze kujenga viwanda vya kuchakata na kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na kilimo, mifugo,nyuki, madini na mazao ya maliasili.
‘’Hadi kufikia tarehe ya leo, maandalizi ya uzinduzi yanaendelea vizuri, ambapo tumealika wawekezaji wakubwa wa ndani wakiwemo Mohamed Enterprises (MeTL), Azania Group, Bakhresa Group, Kahama Oil Mills na Jambo Group of Companies,” alisema Dkt Sengati.
Dkt. Sengati alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Tabora, Taifa na hata Nchi jirani kujipatia nakala ya kitabu hicho cha mwongozo wa uwekezaji wa Mkoa ambacho kitapatikana bure katika tovuti ya Mkoa wa Tabora mara tu baada ya uzinduzi.
Huu ni muendelezo wa kongamano ambalo lilitangulia mwaka 2018, ambapo mwaka huu kauli mbiu ni ‘’Wekeza Tabora kwa Uchumi wa Kijani”.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.