Na Alex Siriyako:
Dkt. Batilda ameyasema hayo leo Aprili 26, katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe hizi ambazo kwa Mkoa wa Tabora zimefanyika katika Viwanja vya Makao makuu ya Brigedi ya Faru, Tabora Mjini.
Dkt. Batilda ameongeza kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaimalika siku hadi siku kwani Serikali ya Tanzania katika awamu zote na zaidi katika awamu hii ya sita imechukua hatua nyingi sana muhimu kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye Muungano ambapo hadi sasa changamoto nyingi sana zimefanyiwa kazi.
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Watanzania ni wamoja na hili linadhihilika kwa muingiliano mkubwa wa kijamii hasa ndoa nyingi sana kati ya Wanzanzibar na Watanzania Bara. Mhe. Batilda ametanabaisha kuwa yeye mwenyewe ni mfano wa ndoa ya Mtanzania Bara na Mzanzibar, hivyo anasema tukiwa na ndoa nyingi sana za aina hii kutakuwa na msingi imara zaidi kwenye Muungano wetu kwani vizazi vya aina hii havina upande wowote zaidi ya kuitwa Watanzania.
Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Tabora amemshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia S. Hassan kwa kuupatia Mkoa wa Tabora fedha nyingi sana za miradi ya maendeleo hasa katika sekta ya Elimu, Afya, Kilimo pamoja na Miundombinu ya Barabara na Reli.
Vilevile pamoja na mambo mengi aliyosisitiza, Mkuu wa Mkoa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote Mkoa wa Tabora kuhakikisha kuwa wanaandaa program maalumu ya kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi wa shule kuanzia Awali mpaka Kidato cha Sita anakuwa na mti wake ambao ameupanda mwenyewe na kuutunza.
Maadhimisho ya Sherehe za Muungano katika Mkoa wa Tabora yamefana sana kwa kushuhudia michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, mpira wa wavu, kukimbiza kuku, Mashindano ya Nsha kwa Wanafunzi wa Sekondari, Mashindano ya Kwaya kwa Wanafunzi wa Msingi na Sekondari, Kuvuta Kamba pamoja na Ngoma za asili.
Katika kuhitimisha maadhimisho haya Wakazi wa Manispaa ya Tabora kupitia Mwakilishi wao ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Mhe. Ramadhan Kapela wamemshukuru sana Mhe. Rais kwa kazi kubwa sana anayofanya kuwatumikia Watanzania na amesema Wanatabora wako naye hatua kwa hatua katika kupigania maendeleo ya Nchi yetu.
MWISHO
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.