Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameagiza kukomeshwa kabisa kwa ukatili wa kijinsia ili kuifanya jamii yote kuishi kwa amani bila kuhofia chochote, na watakaobaimika kufanya hivyo wachukuliwe hatua kali dhidi yao.
Hayo yamesemwa leo kwenye maazimisho ya siku ya kwanza kwenye kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chipukizi vilivyopo Manispaa ya Tabora.
‘’Naaigiza kukomeshwa kabisa kwa ukatili wowote wa kijinsia na kwamba atakaebainika kufanya jambo hilo na kwamba kwa pamoja tukatae mila yoyote potofu itayopelekea ukatili wa kijinsia hasa kwa akina mama na watoto basi achukuliwe hatua kali, na ifike wakati wote tukatae, haiwezekani na kwa pamoja tuseme NO WAY’’, alisema Mwanri.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu aliweka bayana kwamba makundi yanayo athirika zaidi wa vitendo hivyo vya ukatili ni ya wanawake na watoto. Na kwamba upo ukatili wa aina nyingi lakini ukatili wa kimwili kama vile ubakaji, shambulio la kupigwa na mwingine wenye sura kama hiyo huathiri zaidi na hushusha heshima na hadhi ya mtu anaefanyiwa ukatili huo.
Awali akisoma lisara mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Dawati la Jinsia Wilaya ya Tabora Mkaguzi wa Polisi Grace Kaijage, alisema kuwa Dawati la Jinsia wamekuwa wakifanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na idara mbali mbali za Serikali kama vile Idara ya Utawi wa Jamii, Kamati za Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wananwake na Watoto, Mahakama pamoja na viongozi mbali mbali kwenye Serikali za Mitaa.
Hawa wote wamekuwa wakitoa elimu mbali mbali kwa wananchi za namna bora ya kutoa taarifa za unyanyasaji pindi zinapotokea kwenye maeneo yao wanayoishi.
Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni iliyanza tangu mwaka 1991 ikiwa na lengo la kutokomeza aina zote dhidi ya ukatili wa kijinsia, na kwa mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu isemayo kwamba KIZAZI CHENYE USAWA SIMAMA DHIDI YA UBAKAJI
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.