Na Paul P. Kasembo;
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi mbalimbali zikiwamo nguo, mafuta ya kula, mbuzi, na chakula kwa Kituo cha kulelea watoto yatima na wazee wasiojiweza cha Mtakatifu Teŕresia wa Calcuta kilichopo Kata ya Kanyenye na Kituo cha kulelea Wazee Wasiojiweza cha Amani kilichopo Kata ya Mpera hapa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mhe Rais, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi. Dkt. Batilda S. Burian alisema kuwa, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi hizo kwao ikiwa ni sehemu kusherehekea sikukuu yq Krismasi.
"Nimekuja hapa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ametoa zawadi ya Krismasi kwa ajili yenu, na kwamba yeye na Serikali anayoiongoza inawakumhuka na kuwajali sana hivyo nawaomba mpokee," alisema Mhe. Balozi. Batilda.
Utoaji wa zawadi kwa makundi maalumu hasa wakati wa Sikukuu ikiwa ni utaratibu aliojiwekea ili waweze kusherehekea kwa furaha na amani pamoja nao.
=MWISHO=
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.