Na Paul Kasembo - TMC
Naibu Waziri wa Habari, Teknolojia na Mawasiliano Mhe. Eng. Kundo Mathew amefanya ziara katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na kutoa ahadi ya kuboreshwa kwa huduma ya mawasiliano ya simu kwenye baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa na tatizo hilo.
Kauli ya kuboreshwa huduma ilitolewa kwenye Kijiji cha Kipalapala Kata ya Itetemia ambapo pamoja na mmbo mengine, Mhe Kundo alisomewa juu ya kutokuwepo kabisa kwa mawasiliano jambo ambalo limekuwa likihatarisha hata usalama wa enoe hilo sambamba na kusababisha mkwamo kwenye utoaji wa huduma za kijamii.
Awali akifungua mkutano huo wa hadhara Diwani wa Kata ya Itetemia Mhe. Haruna Kulwa alimueleza Naibu Waziri kuwa, eneo hilo limekuwa na tatizo la kutopatikana kwa huduma ya mawasiliano ya simu kwa muda mrefu sana.
Jambo ambalo limepelekea kukosekana kabisa kwa baadhi ya huduma za kijamii na kuhatarisha hata usalama wa eneo lenyewe, hasa pale wanapokuwa na shida ya kuomba hata gari ya wagonjwa, kuomba msaada polisi au kupeana taarifa zozote zile zenye kusudia la tahadhari imekwa ni ngumu sana.
“Suala hili limekuwa la muda mrefu sana Mhe. Naibu Waziri, lakini ujio wako leo huenda kukafungua na kuleta faraja mpya kwa wakzzi wa maeneo haya n vinga vyake, kwakuwa wamesubiria kauli ya Serikali na sasa umefika, nina imani jambo hikli linakwenda kuisha sasa na wananchi watakuwa na amani juu uoatikanaji wa mawasilano”, alisema Diwani Kulwa.
Akimkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Dkt. Yahaya Nawanda alimueleza Naibu Waziri kuwa, Wilaya ya Tabora imejiweka kikamilifu na wapo tayari kwenye utekelezaji wa zoezi ala Anwani za Makazi.
Ambapo kwa Wilaya kuna Kata zote 29, Mitaa 134 na Vijiji 53 kwakuwa mpaka sasa tayari Wenyeviti wote wamepewa semina elekezi pamoja na Watendaji wao na sasa wanasubirira kuanza kwa kazi ambayo waliahidi kufanya kwa uzalendo mkubwa sana.
“Pamoja na shukurani za kuja kutatua kero ya mawasiliano hapa kwetu, pia nikuahidi Naibu Waziri kuwa sisi Wilaya ya Tabora, tumejipanga vizuri sana kwenda kulitekeleza zoezi hikli kwa usahihim kwa wakati na kwa uzalendo mkubwa ili tuweze kuwa wa mfano kwa Mkoa na Taifa pia”, alisema Dkt. Nawanda.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Ndg Robert Makungu alimshukuru sana Naibu Waziri kwa ujio wake hasa kipindi hiki ambapo kuna zoezi la Anwani za Makazi, na kwamba akamuambia kuwa kwa upande wa Mkoa wameelekeza kuanza kutambuliwa na kuwekwa Anwani za Makazi kwa nyumba za viongozi, na majengo yote ya Serikali na hicho ndiyo kipaumbele cha Serikali ya Mkoa.
Akihitimisha baada ya kutembelea Kata ya Itetemia, Ifucha na Kakola Mhe. Naibu Waziri Mhandisi Kundo aliwaahidi wananchi wa hao kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imekuja na suluhisho la tatizo la mawasiliano, ambapo kupitia yeye Naibu Waziri ameahidi kulifanyia kazi kwa haraka ili wananichi waondokane na shida hiyo iliyowakabiri kwa muda sasa.
Aidha alitumia fulsa hiyo kuweleza wananchi hao kuwa, ni wakati wao sas kushiriki vema kwenye zoezi la Anwani za Makazi ili waweze pia kutambuliwa na iwe rahisi kwa Serikali kutatua kero changamoto zao na kuwaletea maendeleo.
Baada ya hili tujiandae sasa kuhesabiwa ili Serikali iweze kupanga mipango yake ya kuleta maendeleo kwa kuzingatia idaidi ya watu wake ambao watakuwa wamehesabiwa, na hilo ndiyonlitakuwa jukumukubwa zaidi la Serikali baada ya ninyi wananchi kuwa mmeshiriki kikamilifu kwenye hayo mambo mawili muhimu.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.