Mwenge wa Uhuru 2022 umezindua Miradi ya Maendeleo miwili ya ujenzi wa Daraja la Upinde wa Mawe lenye urefu wa KM 16.4 lililopo Kjiji cha Kazima, Kata ya Ifucha na ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Sekomdari Kazima iliyopo mtaa wa Boma, kisha kuweka mawe mawili ya msingi katika miradi ya Tabora Polytechnic College kilichopo Kijiji cha Tuli, Kata ya Ifucha pamoja na Kituo cha Afya Misha kilichopo Kata ya Misha vyote vikiwa na thamani ya Tzs 3,037,314,970/=.
Akihitimisha mbio hizo za Mwenge wa Uhuru 2022 Ndg Sahili Nyanzabara Geraruma aliwapongeza viongozi wa Wilaya ya Tabora kwa ushirikiano wao katika kutekeleza miradi ya maendeleo, huku akiwataka kuacha tabia za kutegeana katika utekelezaji wa majukumu hasa kwa upande wa wataalamu wa Manispaa.
Ndugu Geraruma aliwasisitiza viongozi wote pamoja na wataalamu kwenda kuzyatekeleza yale yote yaliyoshauriwa na wakimbiza mwenge kitaifa ili yakawe yenye tija kubwa kwa wananchi wa Wilaya ya Tabora na wananchi wote kwa ujumla kwani miradi hiyo yote inatekelezwa kwa ajili yao.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tabora MHe. Paulo Matiko Chacha aliwashukuru sana wakimbiza Mwenge kitaifa huku akiwaahidi kuwa uongozi wa Wilaya ya Tabora utayafanyia kazi yale yote yaliyoelekekzwa na wakimbiza mwenge kitaifa na kuahidi kuyasimamia maelekezo yote kwa watumishi wote waliotajwa kwenye mbio hizo za mwenge kwenda kuanza Maisha mapya ya utumishi kwa kufuata ushauri uliotolewa
Mwenge wa Uhuru 2022 uliokuwa na ujumbe mkuu usemao ”SENSA NI MSINGI WA MIPANGO, SHIRIKI KUHESABIWA TUYAFIKIE MALENGO YA TAIFA” ulikimbizwa KM 76 ndani ya Manispaa ya Tabora na KM 20 kutoka Tabora Njini mpaka Kijiji cha Ilolangulu kilichopo Wilaya ya Uyui.
MWISHO.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.