Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Tanzania umedhamiria kuzifikia Kata zote za Tabora Manispaa ikiwa ni sehemu ya majaribio (pilot area) kwa Halmashauri zote za Tabora Manispaa.
Hayo yamesemwa leo kwenye kikao na Muwezeshaji kutoka MKUTA TAIFA Bi Rachael alipokutana na Kaimu Mkurugrnzi Tabora Manispaa pamoja na Kamati ya MKUTA Tabora Manispaa kwenye ukumbi wa mikutano Tabora Manispaa.
Bi Rchael akisema kuwa mpaka sasa MKUTA imefanikiwa kupunguza sana ongezeko la wagonjwa wa Kifua Kikuu kwa kuwa kumekuwa na juhudi kubwa ya Serikali kwenye kupambana na ugonjwa huu hatari ambao huenezwa kwa njia ya hewa na mdudu aitwae Mycobacterium tuberculosis complex.
Ugunduzi wa ugonjwa huu huweza kupatikana kwa kufanya vipimo vya makohozi kwa wale walio na kikohozi au sampuli nyingine kulingana nadalili za mgonjwa mwenyewe, ambapo maambukizi yanakadiriwa kuwa chiniya mtu mmoja hadi wane (1-4) wanaweza kuambukizwa na mtu mmoja mwenye TB.
‘’Serikali imeweza kupunguza kwa kiwango kikubwa ugonjwa huu kwa kuwa imewekeza juhudi kubwa kwenye utoaji wa Elimu kwa Umma kupitia vyombo vya habari, vilabu maalumu vilivyoundwa ambavyo huwafikia wananchi kwa makundi mbalimbali na kuwapa elimu juu ya uwepo wa ugonjwa huu hatari na namna bora ya kujikinga nao,’’ alisema Bi Rachael.
Awali akifungua Kikao hicho Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya MKUTA Tabora Manispaa ambaye ni Diwani Kata ya Tambukareli Mhe. Zinduna Kisamba aliwashukuru sana MKUTA pamoja na wafadhiri wote wanaowezesha kupamabana na ugonjwa huo hatari wa Kifua Kikuu.
‘’Kwa mujibu wa takwimu zilizosomwa hapa zinaonesha kupungua idadi ya wagonjwa kwa nchi nzima na Manispaa kwa ujumla, na kwakuwa kuna mpango huu mpya mliokuja nao wakuwafikia wananchi kwenye ngazi zote mpaka kitongoji, sasa niwaagize Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wote kuifanya ajenda hii ya kudhibiti kifua kikuu kuwa ni ajenda ya kudumu kwenye vikao vyote na mikutano kwa ngazi zote mpaka vitongoji,’’ alisema Mhe. Zinduna.
Aidha wajumbe waliitoa ushauri kwa Serikali kwamba kuwepo na Elimu Zaidi hasa kwa wananchi wanaoishi vijijini kwakuwa ndiyo hasa kundi ambalo halipati taarifa kwa wakti, na kwamba kuwepo na muendelezo wa utoaji elimu kwenye kila mkusanyiko hataifike wakati kuwepo na bandas maalumukila maonesho yanayojumuisha wananchi ili kuweza kuifikisah elimu kwa walio wengi Zaidi.
Ushauri mwingine uliotolewa ulikuwa ni kuwepo kwa juhudi za makusudi za kuongeza bajeti kwa ili elimu iweze kutolewa kwa wananchi na iweze kuwafikia wengi Zaidi kwa sababu imefika wakati hata Watoto wadogo nao wanaugua kifua kikuu, na kwamba waitumie pia Ofisi ya Afisa Habari Manispaa ya Tabora ili nayo iweze kusaidia namna bora ya kufikisha elimu hiyo kwa wananchi walio wengi Zaidi.
Serikali imepanga kwamba kufikia mwaka 2030 iwe imetokomeza kabisa ugonjwa wa kifua kikuu, ambapo kwa Tabora Manispaa baadhi ya wagonjwa walibainika kwenye Kata za Ikomwa, Tambukareli na Cheyo.
MWISHO
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.