JUMLA ya shilingi milioni 334 zimetumiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kwa ajili ya ununuzi wa gari la kubeba taka na makontena 20 ya kuweka taka.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Fundi Mkuu wa Manispaa ya Tabora Gaitan Mkeng’e wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani wa Bajeti.
Alisema kuwa gari ni jipya ambalo limenunuliwa kutoka China litasaidia kukusanya na kuondoa takakatika maeneo mbalimbali ya Manispa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Ndunguru alisema uzalishaji wa taka kwa siku katika Manispaa hiyo ni tani 120 lakini kabla ya ununuzi wa gari hilo walikuwa na uwezo wa kukusanya tani 70 kwa siku.
Alisema ununuzi wa gari hilo utawezesha Manispaa hiyo kuwa na uwezo kumalizia sehemu ya taka ambayoilikuwa inabaki kwa siku.
Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira William Mpangala alisema ununuzi wa gari utasaidia sana kwani kila tarafaitakuwa na lake na ukusanyaji wa taka.
Kwa upande wa Diwani waKata ya Cheyo Hamisi Kitumbo alisema ununuzi wa gari lingine itawezesha wakaziwa Halmashauri hiyo kuishi katika mazingira safi na salama.
Alisema hatua hiyoitapunguza kuwepo na uwezekano kwa magonjwa ya mlipuko yanayotokana namrundikano wa uchafu katika maeneo yasiyo rasmi kwa ajili ya kutupa taka.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.