Na Paul Kasembo – TMC
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora leo tarehe 7 Disemba, 2022 imezindua rasmi kampeni ya mwezi wa Afya na Lishe ya watoto katika Zahanati ya Ng`ambo iliyopo Kata ya Kidongochekundu.
Akitoa hotuba ya Mgeni Rasmi, Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora alisema kwamba, kampeni ya Afya na Lishe kwa watoto hufanyika mara mbili tu kwa mwaka yaani mwezi wa 6 na mwezi wa 12 kwa mwaka husika
“Hivyo basi Manispaa ya Tabora kwa kipindi cha mwezi wa 12 imeamua kuzindua hapa katika Zahanati ya Ng`ambo ambapo watoto wenye umri wa miezi 6 – 59 watapewa matone ya Vitamin A, watoto wa umri wa miezi 12 – 39 watapewa dawa za minyoo ya tumbo na watoto wa miezi 12 – 59 watapimwa hali zao za Lishe kwa kutumia MUAC Tape, alisema Jonas Kilave”
Kama lilivyo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa kila Mkoa, Wilaya, Tarafa, Kata, Mitaa na Vijiji kuhakikisha kwamba wanashiriki kikamilifu katika kusimamia na kutekeleza Afua zote za Lishe kwa ajili ya Kuondoa Utapiamlo kwa watoto wote
Jonas Kilave aliwataka Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wote kuendelea kuhamasisha wananchi wote ili waweze kuwapeleka watoto wote walio chini ya umri wa miaka mitano wapatiwe matone ya Vitamini A, dawa za minyoo na kupima hali za Lishe katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya.
“Aidha niwahimize Waganga Wafawidhi wote katika Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwafikia watoto wote na kuwapatia huduma hiyo muhimu Jonas Kilave alisema”
Manispaa ya Tabora inaendelea na utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kuhakikisha kuwa
“Kukuwa kwa watoto wakiwa timamu ki mwili na kiakili ni jukumu la watu wote na msingi mkuu wa kukua vizuri kimwili na kiakili ni LISHE BORA”
MWISHO
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.