Na Paul Kasembo - TMC
Halmashauriya Manispaa ya Tabora imeungana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa kwa kumpongeza mtumishi wake Bi. Tumaini Mgaya ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kutambuliwa utendaji wake na Mhe. Bashungwa kwenye Kongamano la Uwekezaji na Biashara kwa Nchi zilizo jirani na Ziwa Tanganyika.
Mhe. Bashungwa alimtangaza Bi. Tumaini Mgaya kwa kutambua utendaji kazi wake ulio mzuri wenye ubunifu wakati alipokuwa akizungumza na Makundi Maalumu katika Ukumbi wa Chuo cha Uhazili uliopo Manispaa ya Tabora wakati wa Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Katika hafla hiyo Mhe. Bashungwa aliagiza uongozi wa Mkoa na Manispaa kutambua pia mchango wake kwa kumpatia Tuzo ili sehemu ya hamasa na kumtia moyo zaidi yeye mwenyewe pamoja na kuhamasisha watumishi wengine wa Manispaa na Mikoa mingine kuiga mfano wake katika utendaji kazi.
Tukio hilo la utoaji wa Tuzo na Fedha liliongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Mhe. Ramadhani Kapela (Diwani) mbele ya Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Tabora lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Manispaa.
“Sisi Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi, Menejimenti na watumishi wote wa Manispaa ya Tabora kwa pamoja tunaungana na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa kwa kutambua ma kuthami ni utendaji kazi wa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Tabora Bi. Tumaini Mgaya na hivyo tunatekeleza agizo lake hilo kwa kumpatia zawadi ya Ngao na Fedha Tzs Milioni tatu (3) iwe ni motisha kwake na watumishi wengine kuiga mfano wake,” alisema Mstahiki Meya Kapela.
Aidha Mstahiki Meya Kapela alisema kuwa, pamoja na kumpongeza Tumaini haitakuwa vema kama pia hatutatambua mchango anaoupata kutoka kwa watumishi wenzie hasa anaofanya nao kazi kwenye Idara yake.
Hivyo akamuomba Mkurugenzi wa Manispaa kuangalia namna ambavyo anaweza kuwatambua na wao na ikimpendeza kuwapatia Vyeti na angalau kiasi chochote kidogo kwa walio chini ya Mgaya.
Hayo yalijiri kwenye KONGAMANO LA UWEKEZAJI NA BIASHARA KWA NCHI ZILIZO JIRANI NA ZIWA TANGANYIKA baada ya Mhe. Bashungwa kutembelea Banda la Maonesho la Manispaa ya Tabora na kuona kazi za Wajasiliamali wa Manispaa Manispaa hao ambao walikuwa wakiongozwa na Tumaini Mgaya lililofanyika tarehe 9-13 Mei, 2022 Mkoani Kigoma.
Ambapo katika Kongamano hilo, ni Manispaa ya Tabora pekee ndiyo iligharamia na kupeleka wajasiliamali wake kwenye maonesho hayo kulinganisha na Halmashauri zingine.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.