Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imeibuka kinara wa kilele cha maonesho ya nane nane kwa kanda ya magharibi ambayo ilijumuisha Halmashauri 16 kwa Mkoa wa Tabor ana Kigoma.
Akiwapongeza Manispaa ya Tabora wakati wa kufunga maonesho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto Mh. Thobias Andengenye aliwaeleza kwa waende kuyatafisiri mafanikio hayo kwa vitendo ili walengwa wa maonesho hayo ambao ni wakulima na wafugaji wakanufaike na uwepo wao katika kuwapatia elimu ambayo wameitumia hapo kwenye maonesho hata wakaibuka washindi.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi. Dkt. Batilda Buriani aliwaeleza viongozi wa kiserikali, kidini, wadau wa nane nane pamoja na wananchi waiokuwa wamekusanyika katika viwanja hivyo vya nanenane kuwa, Serikali ya awamu ya sita imejipanga vema katika sekta ya kailimo katika kuwahudumia wananchi hasa wakulima na wafugaji kwa kuwapatia teknolojia mpya na ya kisasa itakayo wasaidia wakulima na wafugaji kwenda na wakati ili kuboresha kazi zao ziwe zenye tija maslahi mapana tofauti na ilivyo sasa hivi.
“Mheshimiwa mgni rasmi ninayo furaha kuwajulisha wakulima na wafugaji wa mikoa hii miwili ya Kigoma na Tabora kuwa Serikali ya awamu ya sita imejipanga vema sana katika kuhakikisha kuwa wananufaika na teknolojia mpya naya kisasa katika ufugaji na katika masuala ya kilimo kwa ujumla ili kuwasaidia kuondoka na teknolojia ya zamani na kwamba sasa wanufaike zaidi na mfumo mpya na wapate uchumi mkubwa zaidi”, alisema Dkt. Batilda.
Kando nao, akitoa salamu za Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Mhe. Ramadhani Kapela aliwashukuru waheshimiwa hao wakuu wa mikoa, viongozi wa kiserikali, wadau wa kilimo na mifugo kwa pamoja na wananchi walikuwa wamejaa katika eneo la kilele cha nanenane kuwa, Manispaa ya pamoja inaendelea kujifunza kupitia maonesho hayo.
Na kwamba uwepo wa maonesho hayo katika Manispaa ya Tabor ani fursa kubwa ya kuongeza kipato kwa wananchi wa Manispaa, kujifunza teknolojia mpya na maarifa mapya kutoka makampuni na wadau mbalimbali wa kilimo na ufugaji waliohudhuria na kuonesha taaluma zao hao.
Aidha Mstahiki Meya Kapela alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa kilimo na serikali kuangalia namna bora ya kuanzisha utaratibu wa kupeleka matrekta katika maeneo ya wakulima ili wawe wanapewa huduma hiyo ya kulimiwa mashamba yao na kisha baadae walipe gharama hizo.
Mstahiki Meya aliongeza kwa kusema kuwa, baadhi ya maeneo wanafanya hivyo, na wamefanikiwa zaidi katika sekta ya kilimo kama vile Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara ambapo amekuta kuan utaratibu huo mzuri kwa wakulima.
“Mimi nimelima zao la alizeti katika Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara mbapo kuna huo utaratibu wa mkulima kulimiwa mashamba yake na kisha baadae kulipa gharama hizo, jambao ambalo binafsi limenifanya nilime hekai 500 za alizeti, ni mpango mzuri sana kwa wananchi na unayo tija kubwa,” alisema Mstahiki Meya Kapela.
Akishukuru kwa niaba ya watumishi wote wa Manispaa ya Tabora, Mkuu wa Sehemu ya Kilimo Manispaa ya Tabora Bi Happy Nko, alisema ushindi huo ni wa wana Manispaa kwa ujumla wao maana bila wao na uungaji mkono wao wasingeweza kuibuka na ushindi huo wa kushika nafasi ya kwanza katika kundi la Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa ambazo zilikuwa na jumla ya Halmashauri 16 kwa ikoa yote miwili ya Tabor ana Kigoma.
Maonesho ya nanenane mwaka huu wa 2022 yalikuwa na kauli mbiu isemayo Ajenda 10/30; Kilimo ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.