NaAlex E. Siriyako
LeoJuly 09, 2021, limefanyika zoezi la kihistoria la makabidhiano ya Ofisi ya Mkuuwa Mkoa wa Tabora kati ya Mkuu wa Mkoa mwenyeji ,Mheshimiwa Ally Hapi na Mkuuwa Mkoa mgeni Dkt.Batilda Salha Buriani. Hii ni kufuatia mabadiliko ya uteuziambapo Mheshimiwa Ally Hapi aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na Dkt.Batildakuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora huku akiacha nafasi yake ya ukatibutawala wa mkoa wa Shinyanga.
Tukiohili la kihistoria limefanyika katika ukumbi wa Isike Mwanakiyungi uliopokatika viwanja vya Ofisi za Mkuu wa Mkoa Tabora. Katika zoezi hilo walishuhudiawageni mbalimbali waalikwa wakiwemo; Katibu wa CCM Mkoa Ndugu Solomon Kasapa,Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Tabora, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa waTabora, Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Tabora, Makatibu Tawala,Viongoziwa Dini mbalimbali, Wakuu wa Taaasisi binafsi na za Umma, pamoja na wajumbewengine waalikwa wa makundi tofauti tofauti.
Zoezihilo liliongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Ndugu Msalika Makungu ambaealiongoza utiaji saini hati za makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa , Katibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Ilani ya chama chaMapindizi(CCM) ya 2021/2025.
Katibuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora, Ndugu Solomon Kasapa, katikahotuba yake fupi aliwapongeza Wakuu wa Mikoa hao kwa maana ya Dkt.BatildaBuriani na Ndg.Ally Hapi kwa kuendele kuaminiwa na Serikali ya CCM inayoongozwana Mama Samia Suruhu Hassan. Kikubwa zaidi amewaasa wakawe viongozi na siowatawala katika maeneo yao na watumie muda wao mwingi kutatua kero za wananchi.
NduguAlly Hapi, ambae kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, alikuwa Mkuu wa Mkoa waTabora kwa siku ishirini na tano, alipata wasaa wa kusema yake machache ambapoalimpongeza Dkt.Batilda kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.Amewaomba wana Tabora, ikiwemo Sekretarieti ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Viongoziwa Dini, na wanachi wa Tabora kumpa ushirikiano mkubwa Dkt.Batilda ili awezekuleta maendeleo yaliyokusudiwa mkoani Tabora.
Kwaupande wake Dkt.Batilda Buriani , kwanza alimshukuru Mungu, alimshukuru MamaSamia Suruhu Hassani kwa kumwamini na na aliwashukuru wananchi wa Tabora kwaujumla kwa mapokezi makubwa na mazuri waliyompa. Ameahidi kwenda kupiga kazivyema baada ya kukabidhiwa vitendea kazi ambavyo ni pamoja na Hati yamakabidhiano, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Ilani yaChama cha Mapinduzi.
Dkt.Batildaameahidi kuwa atakuwa mnyenyekevu kwa wanachi, anaenda kutatua kero za Wananchiwa Tabora, lakini hatosita kuwachukulia hatua watendaji wa Serikali wazembe nawasio waaminifu.
Piaalihitimisha hotuba yake fupi kwa kuwaomba wananchi wa Mkoa wa Tabora kuchukuatahadhari dhidi ya ugonjwa wa CORONA (COVID 19), ambaokwa sasa Dunia inakabiliana na wimbi la tatu la ugonjwa huo. Amewataka wanchiwachukue tahadhari zote za kiafya ikiwemo kuvaa barakoa, kunawa mikono kwasabuni mara kwa mara, matumizi ya sanitaiza, pamoja na kuepuka misongamanoisiyokuwa ya lazima.
MWISHO.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.