Tume ya Haki Za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imefanya semina ya siku mbili na Madiwani wa Halimashauri ya Manispaa ya Tabora ambayo ilihudhuriwa na Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Tabora, Ndg Rukia Manduta,Waheshimiwa Madiwani wa Halimashauri ya Manispaa ya Tabora na Wanahabari wa vyombo mbalimbali.Katika semina hiyo yenye mada ya “ Haki za Binadamu na Utawala Bora”, Madiwani wanatarajiwa kujengewa uwezo wa kuwa na weredi wa kutosha kuhusiana na haki za binadamu na utawala bora.
Miongoni mwa mada ndogo ndogo zilizowasilishwa ni pamoja na Historia ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora(THBUB). Hii iliwasilishwa na Ndugu Ayoub Msendo Mackanja, ambae alieleza kuwa THBUB ni Idara huru ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa ibara 129(1) ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano ya mwaka 1977, kwa lengo la kukuza na kulinda hifadhi ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora Nchini Tanzania.
Haki za Binadamu ni miongoni mwa mada zilizowasilishwa katika semina hii vile vile. Mada hii ikiwasilishwa na Ndugu Paul Sulle, alieleza kwamba kimsingi haki za binadamu ni uhuru muhimu alionao binadamu kwa sababu tu yeye ni binadamu. Ameeleza zaid kwamba duniani wimbi la haki za binadamu lilikuwa kubwa hususani baada ya vita kuu ya kwanza ya Dunia mwaka 1914-1918, lakin haki za binadamu zikajengeka zaid kidunia kwa mwogozo wa makubaliano ya mikataba miwili ambayo ni Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa(ICCPR), na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamadunu(ICESCR) ambazo kwa pamoja zinaunda Hati ya Kimataifa ya Haki za Binadamu(International Bill of Rights).
Dhana ya Utawala Bora ni moja miongoni mwa mada zilizowasilishwa vilevile katika semina hiyo. Mada hii ikiwasilishwa na ndugu Mbwana Mussa Mbwana, ambaye alieleza maana halisi ya Utawala Bora kuwa ni zoezi la wenye madaraka katika maamuzi kuamua ni namna gani rasilimali za Taifa zitumike kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi.
Ameeleza zaidi kwamba kimsingi Utawala Bora misingi yake ni uwazi, uwajibikaji, utawala wa sheria, ushirikishwaji,usawa, ufanisi na tija, mwitikio, maridhiano pamoja na uadilifu. Alifafanua zaidi kwamba katika hali ya kawaida sana, misingi hiyo ikitekelezwa, utawala bora umetekelezwa na hali kadhalika isipotekelezwa hakuna utawala bora.Utawala Bora huleta matumizi mazuri ya rasilimali za nchi, maendeleo endelevu, huduma bora za jamii na kuheshimiwa kwa haki za binadamu.
Mada ya Serikali za Mitaa ni moja ya hoja zilizowasilishwa katika semina hiyo, akiwasilisha mada hiyo Mwanasheria wa Halimashauri ya Manispaa yaTabora ndugu Deodoroth Chuwa,ambaye alieleza kwa mapana maana,historia na chimbuko la serikali za mitaa, alieleza nafasi za watendaji wa kata na madiwani katika kuleta maendeleo yenye tija kwa kata zao. Alifafanua majukumu ya Diwani na mipaka yake pamoja na Afisa mtendaji kata, na umuhiimu wa wao kuwa kitu kimoja katika kutekeleza utawala wa Sheria unaozingatia haki za raia.
Aidha Madiwani waliweza kuibua changamoto mbalimbali zikiwemo za ukiukwaji wa haki za binadamu katika meneo mengi ndani na nje ya Manispaa ya Tabora, changamoto za kiutendaji kwani wanadai mamlaka waliyonayo ni madogo , hawawezi kuwawajibisha kinidhamu papo kwa papo watendaji wa Serkali wanaotumi vibaya madaraka yao. Vilevile walieleza suala la wenyeviti wa vijiji kukosa posho wakati watendaji wa vijiji wana mishahara, hivyo ufanis wa wenyeviti na uaminifu unakuwa changamoto sana katika kuleta maendeleo endelevu.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.