BAADHI ya Vyama vya Siasa MkoaniTabora vimelipongeza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kwa kutokuwa na makundi na kuwa na mshikamano na umoja wakati wa uendeshaji vikao vyake.
Kauli hiyo imetolewa jana na viongozimbalimbali wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi(CUF) walioalikwa kuhudhuria kikao maalumu cha Baraza hilo.
Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Tabora Msabaha Kambambovu alisema uendeshaji wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaaya Tabora na uchangiaji wa Madiwani umeonyesha kuwepo na umoja miongoni mwao licha ya viongozi hao kutoka Vyama tofauti vya kisiasa.
Alisema katika muda wote alipokuwa ndani ya ukumbi wa mikutano hakuona zomeazomea wala mjumbe kukatazwa kuchangia kwasababu ya utofauti wake wa kisiasa.
Kambambovu alisema ni vema waendeleze mshikamano huo kwa ajili ya maslahi mapana ya kuwasaidia wakazi wa Manispaa ya Tabora.
Naye Mwenyekiti wa CUF Wilaya yaTabora Mirambo Camil alisema kama ni mgeni wa Madiwani waliopo katika Barazahilo unaweza kudhani wanatoka Chama kimoja kwa jinsi walivyokuwa wakishirikiana katika uchangiaji wa hoja mbalimbali.
Alisema umoja huo utasaidia kuijengaTabora mpya ambayo itapeleka miradi ya maendeleo katika maeneo yote bila kujali Diwani wa Kata husika anatoka upinzani.
Naye Mtahiki Meya wa Manispaa yaTabora Mh. Leopold Chundu Ulaya aliwataka Madiwani wote kuendeleza Umoja na mshikamano ili waweze kusaidia katika kuwaletea maendeleo wakazi wa eneo hilo.
Alisema kuwa hata Mheshimiwa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anasema maendeleo hayana Chama kwa hiyo ni vema wakaendeleza umoja ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Katika hatua nyingine Baraza laMadiwani la Manispaa ya Tabora limepitisha mapendekezo ya marekebisho ya bajeti ya ruzuku ya miradi ya maendeleo ya miundombinu (LGCDG) ya bilioni 1.3 kwa ajili ya mwaka huu wa fedha (2017/18).
Mapendekezo ya marekebisho ya bajeti hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bosco Ndunguru katika kikao cha dharura cha Baraza hilo.
Alisema wameamua kufanyika marekebisho hayo kufuatia agizo la Waziri wa Nchi Ofisi yaRais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa za kuzitaka Halmashauri zote nchini kufanyia uchambuzi upya bajeti za miradi ili kuwa na miradi michache inayotekelezeka na kukamilika kwa wakati na kwa asilimia 100.
Mkurugenzi huyo Mtendaji alisema kuwa inalenga kuongeza wingi na ubora wa huduma za jamii na miundombinu pamoja na kuwezesha utawala bora.
Ndunguru alisema miradi itakayotekelezwa ni ile inayohusu sekta ya afya na elimu ambayo ujenzi wake umefikia katika mtambaa panya na miradi hiyo inatakiwa kukamilika kabla ya mwaka huu wa fedha kumalizika.
Aliongeza miradi mingine itatekelezwa katika Bajeti ya mwaka ujao wa fedha kulingana na upatikanaji wa fedha
Mwisho
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.