Angalizo hilo limetolewa na mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2019 Mzee Mkongea Ali baada ya kukagua mradi wa “Ujenzi wa Mtandao wa barabara zenye urefu wa KM 5.32 kwa kiwango cha Lami” uliopo kata ya Ipuli na Mpera Manispaa ya Tabora, ambayo imejengwa na mkandarasi wa kampuni ya Chongqing International Constraction Corporation (CICO) na Mkandarasi Mshauri wa mradi ni Advance Engineering Solutions.
Ali alisema kwamba Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikijikita kwenye kuleta maendeleo chanya kwa Watanzania wote jambo ambalo ndiyo ilikuwa kiu kubwa kwa wananchi nchini kote.
Ndiyo maana naanza kwa kuwataka Wana Manispaa wote kwamba wanapaswa kuilinda miradi yote iunayojengwa kwenye makazi yao na kwa kuzingatia kwamba miradi hiyo ni mali yao na inatokana na kodi zao wao wenyewe Watanzania.
“Japokuwa kipande hiki bado kinaendelea na ujenzi lakini nasema kazi ni nzuri sana na kwamba pongezi za dhati zimuendee Mhe Rais Joseph Pombe Magufuli kwa kuamua kuweka lami, kwa kuwa ni ahadi zake kuziweka barabara kwenye hadhi ya lami” alisema Mzee.
Aidha aliwapongeza wataalamu wote kwa kusimamia kazi hiyo kwa weredi wa hali ya juu sana mpaka kuonesha thamani ya pesa/ value for money.
Kukamilika kwa Mradi huu wa barabara yenye urefu wa KM 5.32 utakaogharimu zaidi ya kiasi cha shilingi Bilioni sita, kunaleta manufaa makubwa zaidi kwani sasa wananchi wanaweza kupita nyakati zote yaani masika na kiangazi, kuongeza thamani ya maeneo yaliyokaribu na barabara hizo, kupitisha mizigo na abiria na wakati wa ujenzi wana Manispaa wapatao 182 wanapata ajira za wakati wa ujenzi wa barabara hiyo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Ali alikagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Manispaa ya Tabora ipatayo mitano yenye zaidi Bilioni nane, ambapo mmoja kati ya miradi hiyo ulikataliwa ambao ni wa umaliziaji wa ujenzi wa madarasa mawili Sekondari ya Chang’a Tumbi.
Kisha baadae Mzee aliongea na wananchi kwenye uwanja wa Chipukizi na kisha alipewa nafasi ya kutoa hundi ya mfano yenye thamani ya shilingi milioni 110 kwa vikundi vya wajasiliamali 21 vya wanawake 10 sawa na mil 50, vijana 8 sawa na mil 45, walemavu 3 sawa na mil 15 pesa hizo tayari walishawekewa kwenye akaunti zao na akawataka kwenda kuzifanyia kazi iliyokusudiwa na kuhakikisha kwamba wanarejesha kwa wakati ili na wengine wapate nafasi ya kukopeshwa.
Akihutubia wananchi waliofurika viwanja vya Chipukizi Mzee alisema kuwa Manispaa ya Tabora na Mkoa kwa ujumla wamepata bahati ya kuwa na Mradi mkubwa wa Maji ya Ziwa Victoria hivyo akaisisitiza jamii ya wana Tabora kuwa inawajibu mkubwa kuvitunza vyanzo vya maji na mindumbinu yake .
Alisema kwamba serikali inawajali wananchi wake ndio maana inatekeleza mradi huo mkubwa katika mkoa wa Tabora ambapo zaidi ya wananchi milioni 1 watanufaika na maji hayo.
Alisema kwamba serikali kupitia kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani na huo ndio utekelezaji wake ili wananchi wanufaike na taifa lao.
Alisema kupitia kauli mbiu ya mwenge mwaka huu inayosema “maji ni haki ya kila mtu ,tuvitunze vyanzo vya maji
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imetoa mamilioni ya fedha kwa halmashauri zote hapa nchini ili kuboresha miundombinu na huduma mbalimbali za kijamii hivyo akawataka wadau wengi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo ili kuwezesha upatikanaji wa huduma bora zkatika maeneo yote hapa nchini
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.