Na Paul Kasembo
Kikao cha Kamtiya Afya ya Msingi kimefanyika katika Wilaya ya Tabora hukukikisisitiza elimu kuendelea kutolewa kwa wananchi wote wa Wilaya iliwawe na uelewa wa pamoja kwa muktadha mpana wa kuondoka na matatizoyatokanayo na Afya ya Msingi.
Akisoma hotuba kwa wajumbe wa kamati hiyo Bi. Haika MasueakimuwakilishaKaimu Mkuu wa Wilaya ya Tabora ambaye pia ni Mkuu waWilaya ya Tabora Mhe. Paul Chacha Matiko alisema kuwa Wilaya yaTabora imepokea Dozi Sitini natatu elfu (63,000) ya chanjo ya tone yaPolio ambazo tayari zimesambazwa katika Vituo vyote vya kutoleahuduma za Afya.
Bi Haika alisema kuwa Kampeni hii imelenga kuwafikia watoto Hamsinina mbili elfu na mia nne themanini na sita (52,486) wenye umri wachini ya miaka mitano (5) kampeni ambayo itafanyika kwa utaratibu wakupita nyumba kwa nyumba, vituo vyote vya kutolea huduma za afya,maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi kama vile vituo vya kuleleawatoto wadogo, stendi za mabasi, sokoni na minadani.
“Hadi sasa maandalizi yote ya utekelezaji wa kampeni hiiyanaendelea katika ngazi zote kuanzia Wilaya, Vituo vya kutoleahuduma ya Afya na katika shule zote za Msingi, hivyo nitoe wito kwaMkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Wanahabari, Viongoziwa Kijamii, Viongozi wa Madhehebu ya Dini na wadau wengine katikakuhakikisha kuwa ujumbe unawafikia walengwa kwa uhakika na kwawakati,” alisema Haika.
Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi muwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaaambaye pia ni Mkuu wa Divisheni ya Elimu Msingi Bw. Joel A. Mkuchikaalisema kuwa Manispaa ya Tabora imejipanga vya kutosha katikakutekeleza zoezi hilo muhimu kwa maslahi mapana ya watoto na jamii yaManispaa ya Tabora kama ambavyo Serikali imeelekeza.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.