ya fedha na Utawala ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Msatahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Mhe. Leopord Ulaya leo tarehe 23/09/2019 imetembelea na kukagua ujenzi wa mtandao wa barabara za lami zenye urefu wa km 5.32.
Akizungumza baada ya ukaguzi huo Mhe Ulaya alisifu juhudi zinazofanywa na mkadarasi (Chongoging International Construction Corporation (CICO) chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Manispaa ya Tabora.
“Nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya kwenye ujenzi huu wa barabara ya lami na kwamba imeonesha matumaini makubwa ya kwamba kazi hii itaisha kwa wakati na kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi wa Manispaa yetu ya Tabora kwa kuwa sasa wataweza kupita wakati wote na kupitisha bidhaa zao na hivyo kuwa na uhakika wa kukua kwa uchumi kwa wananchi wote na kubadilisha mandhari ya muonekeano wa Manispaa yetu, alisema Ulaya’’.
Kwa upande wake Onesmo Mgoha ambae ni Mhandisi mshauri wa kampuni ya Advanced Enginnering Solution Ltd aliwaeleza wajumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala kwamba ujenzi unaondelea unazingatia vigezo na masahrti yote ya kikandarasi na kwamba ujenzi huo upo kwenye ubora wa hali ya juu kabisa na hauna shaka yoyote.
Awali kwenye utambulisho wa wajumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala Mhandisi Edwin Kabwoto ambaye ndiye Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini kwa Manispaa ya Tabora aliwaeleza wajumbe kuwa Mhandisi mshauri yupo eneo la ujenzi (Site) wakati wote na anaendelea na kazi bila kuchoka ili aweze kukabidhi kazi kwa wakati.
Ujenzi wa mtandao wa barabara za lami kwa Manispaa ya Tabora unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2019
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.