Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imetembelea na kukagua Miradi mbalimbali ikiwemo ya vyanzo vipya vya mapato ilikujione namna ambayo inaendelea kutekelezwa.
Akizungumzawakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Leopord Ulaya ambaye ndiyeMstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora, alisema pamoja na kuridhishwa kwa namnaambavyo Miradi inatekelezwa, lakini pia aliagiza Menejimenti kutafuta ufumbuziwa changamoto zilizojitokeza na zinazojitokeza ili kuweza kutoa huduma iliyobora zaidi kwa wananchi wa Manispaa ya Tabora.
“Pamojana kuridhishwa na Menejimenti kwa namna ambavyo mnasimamia na kutekeleza miradihii yote ambayo inaendelea na inayoaanza katika sekta zote na ule mradi mpyautapelekea kuongeza mapato ya Halmashauri mfano kuwekwa kwa geti stendi ya basiambapo wale wote wasiokuwa na tiketi ya basi na wananingia stendi kuapatahuduma watapaswa kulipia Tshs 200/=kwa mtu mmoja. Lakini pia tunaagiza kuona namnaya kushughurikiwa kwa changamoto zote zilizo tajwa ikiwemo ya kujenga sehemu yakupumzikia abiria, sehemu ya kujikinga wakati wa mvua hasa kwa wale watumishiwaliopo kwenye geti zote tatu pale stendi, na upatikanaji wa madawati kwamadarasa mapya yaliyokamilika’’, alisema Mhe Ulaya.
Aidhakwa upande wake Naibu Mstahiki Meya Manispaa ya Tabora Mhe Yahya Mhamalialiwataka wataalamu wote wa Manispaa ya Tabora kufanya kazi kwa weledi naubunifu ili waweze kuisaidia Halmashauri ya Manispaa kuongeza Mapato, jamboambalo litaleta mrejesho wa huduma iliyobora zaidi kwa wananchi wote waManispaa ya Tabora.
Awaliakitoa taarifa ya Miradi, Mchumi wa Manispaa Ndugu Joseph Kashushura aliwaelezawajumbe wa kamati kuwa kwa sasa Menejimenti ya Manispaa ya Tabora inaendeleakwa kasi zaidi kutekeleza Miradi iliyopo na kuanzisha Miradi mingine ambayoitakuwa ni vyanzo vipya vya mapato ya Halmashauri kama vile kuwekwa kwa getistendi ya basi ambapo kwa siku makusanyo ni zaidi ya laki sita na wastani waMillioni 4 kwa wiki inapatikana kwa sasa na hivyo kuwa na ongezeko la kati yaasilimia 5 mpaka 6 kwenye pato la ndani la Halmashauri ya Mnispaa yaTabora.
Kamatiya Fedha na Utawala ya Manispaa ya Tabora ilitembelea na kukagua miradi kadhaaikiwemo ukarabati wa Machinjio, chanzo cha kipya cha mapato cha stendi ya basi,ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa KM 6.2 na ujenzi wamadarasa kwa shule za msingi.
Kuanzishwa,kuboreshwa na kusimamiwa vizuri kwa miradi hii kutasaidia sana kuongeza mapatokwa Serikali na kwa wananchi wa Manispaa ya Tabora na hatimae kuwezesha utoajiwa huduma zilizo bora na zenye tija zaidi hasa kwenye sekta za Afya, Elimu,Miundombinu, Maji na kupunguza mlundikano wa wanafunzi kwenye madarasa.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.