Pongezi hizo zimetolewa leo na Hannah Kim kiongozi wa timu ya World Bank Supervion Mission Group Two alipotembelea Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ili kukagua utekelezaji wa Mradi huo wa ULGSP.
Sifa hizo zilielekezwa kwa Menejimenti yote ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ambayo inaongozwa na Bosco Ndunguru ambae ndiye Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora, kuwa wametekeleza Mradi huo kwa ubora, viwango na kwa wakati stahiki jambo ambalo lilimfuarahisha sana Kim.
Sambamba na ukaguzi wa miradi hiyo ya ULGSP lakini pia alipata fulsa ya kutembezwa na kuona maeneo mbalimbali itakapojengwa miradi mingine kama vile Dampo la kisasa, Machinjio ya kisasa eneo la kata ya Kitete na kata ya Ng’ambo pia na mradi wa ujenzi stendi ya basi ambayo itakuwa ya kisasa zaidi kwenye eneo lilipo kata ya Ipuli hapa Manispaa ya Tabora.
Kwa upande wa wataalamu waliokuwa wameongozana na ujumbe huo Mhandisi Rashid Mtamila na Muindi Mushangi waliipongeza Menejimenti yote ya Manispaa ya Tabora kwa kuwa wameweza kutekeleza kwa ufanisi, weledi na umakini mkubwa na tena kwa wakati na hivyo kuifanya Manispaa ya Tabora kuwa na muonekano wa kisasa zaidi na wenye mvuto na wenye thamani inayolingana na matarajio yao.
Awali akiwakaribisha wajumbe hao kutoka Benki ya Dunia, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Bosco Ndunguru aliwaeleza wajumbe kuwa Manispaa ya Tabora imefanya vizuri sana kwenye utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa barabara zenye jumla ya urefu kwa KM 21.35, ununuzi wa mitambo mine (4), kontena za kutunzia taka ngumu arobaini (40) na lori mbili (2).
Vyote hivyo kwa pamoja vinaifanya Manispaa ya Tabora kwa sasa kuonekana ya kisasa zaidi na yenye mandhari ya kuvutia sana hasa ukizingatia pia kumefanyika upandaji miti pembezoni mwa barabara zote zoezi ambalo lilikuwa likisimamiwa na Agrey Mwanri Mkuu wa Mkoa wa Tabora pamoja na Komanya Kitwala Mkuu wa Wilaya ya Tabora. Na hivyo kuifanya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kuwa ni moja kati ya Halmashauri zinazofanya vizuri zaidi kati ya zile zinazotekeleza Miradi ya ULGSP Tanzania Bara,‘’alisema Ndunguru’’.
Ziara hiyo pia ilijumuisha wataalamu mbalimbali kutoka OR-Tamisemi, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Tarura Manispaa, Kampuni ya ujenzi wa barabara CICO, na Kampuni ya Mhandisi Mshauri-Advance Engineering Solution.
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ni miongoni mwa Halmashauri kumi na nane (18) Tanzania Bara inayotekeleza Miradi ya Uboreshaji Miji na Manispaa (ULGSP).
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.