Na Alex Siriyako:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Tabora leo juni 6, 2023.
Dkt. Mpango kabla ya kuweka jiwe hilo amefanya ukaguzi wa majengo ya Hospitali hiyo na kujiridhisha juu ya ubora wa miundombinu hiyo ukiringanisha na fedha ambazo zimetolewa na Serikali ikiwa ni pamoja na kupanda mti wa historia ya uwekaji jiwe la msingi katika Hospitali hii.
Akipokea taarifa ya ujenzi wa Hospitali, Dkt. Mpango ameelezwa kuwa jumla ya bilioni 2.88 zimepokelewa kutoka Serikali kuu kwaajili ya ujenzi wa majengo 13 kwa awamu tano tofauti.
Baada ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Hospitali hii, Dkt. Mpango ametoa maelekezo ya Serikali;
Ameelekeza Serikali ya Mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na TAMISEMI pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora wahakikishe ujenzi wa Hospitali hii unakamilika mapema sana kadri itakavyowezekana.
Amewataka Watumishi wa Umma kufuata sheria, kanuni na taratibu hususani kwenye manunuzi ya Mali za umma, na akaongeza kuwa yeyote atakayekiuka sheria na taratibu hizi sheria zichukue mkondo wake.
Mwisho wa hotuba yake kwa wakazi wa kata ya Mpera, Mhe. Mpango amewashukuru sana kwa mapokezi yako, amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa fedha nyingi anazotoa kwenye miradi ya maendeleo hususani Sekta ya Afya, na zaidi ameahidi kufanya ziara ya kikazi Mkoani Tabora kabla ya Disemba ya mwaka huu.
Mwisho
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.