Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (AFYA) Dkt. Festo Dugange, ameagiza ujenzi wa shule mpya za sekondari na msingi uzingatie miundombinu ya michezo kwa wanafunzi. Aidha amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kutenga maeneo ya michezo wanapopanga na kupim miji yao ili iendane na mahitaji ya wakati husika.
Akifunga mashindano hayo ya UMISSETA na UMITASHUMITA TAIFA 2022 Dkt. Dugange amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inatambua umuhimu wa michezo na ndiyo maana imeamua kuendeleza kwa wanafunzi hao kushiriki ili kuendeleza vipaji vya watoto hao.
Aidha kuhusu suala la upungufu wa waalimu wa masomo ya michezo Dkt. Dugange alisema anawahakikishia kuwa Serikali imejipanga kuongeza ajira za kada ya ualimu kwa masomo yote wakiwemo waalimu wa michezo kwa sahule za msingi na sekondari.
Na katika kuimarisha usimamizi wa shughuli za michezo, Sanaa na utamaduni katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Serikali imeanzisha Kitengo cha Utamaduni, Sanaa na Michezo kuanzia Julai 1, 2022.
“Changamoto za Halmashauri kutokuwa na Maafisa Utamaduni na Maafisa Michezo Ofisi ya Rais – TAMISEMI tutashirikiana na wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo na Wizara ya Utumishi ili kuzifanyia kazi changamoto hizo zilizopo na Kitengo hiki kuimarika ili kuzifanikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Sita,” alisisitiza Dkt. Dugange.
Kando nae, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda S. Burian ameishukuru sana Serikali ya Awamui ya Sita kwa kuamua kuuchagua Mkoa wa Tabora kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, na kwamba michezo hiyo imekuwa na tija kubwa sana kwa wanafunzi wenyewe, waalimu imleta furaha kubwa miongoni mwao na kuimarisha upendo sambamba na kuinua uchumi wa Mkoa kwa ujumla kwani wajasiliamali wadogowadogo, wakubwa na wote kwa pamoja wamefanikiwa kufanya biashara zao vizuri kabisa.
Kufungwa kwa mashindano haya, kunafungua fursa nyingine ya mashindano kwa shule za msingi Afrika Mashariki yatakayoanza mwishoni mwa mwezi huuwa Agosti katika Jiji la Arusha.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.