Na Paul Kaembo-TMC.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Buriani ameipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Tabora –TUWASA kwa kuweza kufikia asilimia tisini na mbili (% 92) ya utoaji wa huduma ya maji safi kwa wananchi wa Halmashsauri ya Manispaa ya Tabora ambapo jumla ya Kata 24 kati ya Kata 29 zinapata huduma ya maji.
Pongezi hizo amezitoa wakati wa ziara yake ya kikazi alipotembelea TUWASA na kukagua vyanzo mbalimbali vya maji vilivyopo hapa Manispaa ya Tabora ikiwamo Bwawa la Igombe, Tanki la maji –Itumba na Tanki za maji zilizopo Filta baada ya Mkurugenzi wa TUWASA Mhandisi ……kusoma na kwasilisha taarifa ya Mamlaka kwake Dkt. Batilda.
“Niwapongeze sana TUWASA kwa namna ambavyo mmeweza kuongeza wigo wa utoaji huduma kwa wananchi wote hasa wa Manispaa ya Tabora ambapo mmefikia asilimia 92 sawa na Kata 24 kati ya Kata zote 29 zinazounda Halmashauri ya Manispaa ya Tabora jambo ambalo ni jema sana kwa muktadha wa TUWASA na wananchi wa Manispaa kwa ujumla kwenye hili mnastahili pongezi,” alisema Mhe. Dkt. Batilda.
Awali akiwasilisha taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhandisi ….. alisema kuwa pamoja na mafanikio ya kuweza kutoa huduma kwa asilimia 92, lakini pia wameweza kuunganisha mfumo wa maji taka kwa jumla ya wateja 482, kupatikana kwa huduma ya maji masaa 22 kwa siku, jumla ya tanki za maji saba zipo hapa Manispaa ya Tabora, na kubadilisha mtandao wa bomba za muda mrefu na kuweka mfumo wenye bomba za kisasa zaidi.
Kando na mafanikio hayo, Mamlaka inapitia changamoto kadhaa ikiwamo hujuma kwa miundombinu yake hasa ya mtandao wa bomba zilizochimbiwa chini ya ardhi ambapo mara nyingi hukatwa, gharama kubwa ya utoaji wa huduma ya maji kutoka Ziwa Victoria kulinganisha na maji yanayopatikana kwenye bwawa zilizopo hapa Manispaa ya Tabora. Matumizi ya kibinadamu kwenye vyanzo vya maji, uchafuzi wa mazingira, na kutolipa ankara kwa wakati kutoka kwa watumiaji wa huduma.
Aidha Mhandisi ….. alibainisha baadhi ya mikakati waliyonayo Mamlaka ili kuwafanya wateja wao waendelee kufarahia huduma yao ikiwa ni pamoja na kuhahaikisha kuwa wanapunguza gharama za uendeshaji huduma ya maji toka Ziwa Victoria, kudhibiti upotevu wa maji angalau ifikie asilimia 26 kati ya 36 zilizopo hivi sasa, kushirikisha wadau kwenye kazi na utekelezaji wa shughuri za Mamlaka ili kupata mtazamo wao namna ya kuboresha huduma, kuimarisha makusanyo na kuongeza wateja zaidi kwa kuwa hivi sasa maji ni mengi kulinganisha na awali.
Kwenye ziara hii Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Buriani aliongozana na Katibu Tawala wa Mkoa Ndg Msalika Makungu, Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Dkt. Yahaya Nawanda na baadhi ya watumishi wa Serikali.
MWISHO
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.