Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini Komanya Kitwala leo amegawa Kadi za Bima ya Afya (CHF ILIYOBORESHWA) kwa watoto 228 wenye mahitaji maalumu wanaosoma kwenye Shule za Msingi Viziwi na Furaha zote za Tabora Manispaa.
Kadi hizo za Bima ya Afya zimegharimiwa na shirika la Caritas linalomilikiwa na Kanisa Katoriki Jimbo kuu Tabora ambazo zitaweza kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalumu kupata huduma ya matibabu kuanzia ngazi ya Zahanati mpaka hospitali ya Rufaa popote pale hapa nchini.
Akizungumza wakati wa haflaya kukabidhi kadi hizo kwa wanafunzi hao, Mkuu wa Wilaya alisema kuwa ni vema sasa tuwe na mguso kwa mtu mmoja mmoja, mashirika ya kiserikali au yale yasiyokuwa ya kiserikali kuweza kuwasaidia wanafunzi na wale wasikuwa wanafunzi hasa wale wenye mahitaji maalumu kama hawa ili na wao wahisi wapo kwenye jamii inayowajali na kutambua uwepo wao. Kwa kufanya hivyo kutakuwa na msaada mkubwa sana kwa jamii zetu, serikali na hazina kubwa kwa Mwenyezi Mungu pia.
“Ninawashukuru sana Shirika la Caritas ambalo limejitolea kuwalipia gharama za Kadi hizo zote kwa wanafunzi hawa ambapo leo hii ndiyo nawakabidhi wanafunzi hawa wenye mahitaji maalumu kutoka Shule ya Msingi VIziwi, na Shule ya Msingi Furaha ambayo inafundisha wanafunzi wasioona. Nitumie fulsa hii kuwaomba wahisani wengine yakiwemo mashirika ya kiserikali na yasiyokuwa ya kiserikali kuiga mfano huu wa shirika la Caritas, aidha nimshukurui pia Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Tabora Tumaini Mgaya ambaye alishiriki kuandaa kazi hiyo yote.” Alisema Komanya.
Kwa upande wake Sheikh wa Wilaya ya Tabora Mjini Ramadhani Juma alimshukuru sana Mkuu wa Wilaya kwa kutambua uwepo wake na hata akamualika kwenye hafla hiyo, pia akatumia fulsa hiyo kuwapongeza Caritas kwa namna walivyoguswa hata wakaamua kugharamia kadi hizo za Bima ya Afya. Kisha akatumia fulsa hiyo kuwaomba wahisani wengine kuweza kujitokeza kuwasaidia watoto hasa wenye mahitaji maalumu waweze kuhisi kuwa tupo pamoja, maana kwa hali waliyonayo kwa sasa ni kama yatima vile, hivyo tushirikiane kuwasaidia na tusiwaachie peke yao shule husika klwa hao watoto ni wetu sote.
Naye Mch. Marco Ngalu wa Kanisa la AICT TABORA, aliwapongeza sana wadau wote akianzia na Mkuu wa Wilaya kwa namna ambavyo amekuwa akisaidia shughuri nyingi za kijamii ikiwemo hii ya leo ya kukabidhi kadi za bima ya afya kwa wananfunzi hawa wenyewe mahitaji maalumu wa Shule hizi za Msingi Viziwi na Furaha. Lakini pia alitumia fulsa hiyo kuwaomba wadau wengine mbali mbali waweze kujitokeza kuwasaidia wanafunzi hao ambao kwakweli wanahitaji ukaribu zaidi muda wote.
Kukabidhiwa kwa kadi hizo kwa wanafunzi hao wa shule za msingi Viziwi na Furaha kutawapatia uhakika wa matibabu ya afya na hivyo kuwawezesha kusoma na kwa uhakika na hatimae kuongeza ufaulu zaidi kwakuwa watakuwa na afya njema wakati wote.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.