Na Alex Siriyako:
Maagizo haya ameyatoa leo Machi 15, 2023 katika kikao cha tathimini ya hali ya lishe kwa robo ya pili (Octoba-Disemba) ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.
Vikao kama hivi hufanyika kila robo ya mwaka kwa lengo la kutathimini hali halisi ya lishe kwa Wakazi wa Manispaa ya Tabora. Na ili kupata taswira halisi , wajumbe wanapata fursa ya kutathimini kiashiria kimoja baada ya kingine kwa kulinganisha na utekelezaji wake kwa maana ya jitihada za kuhamasiha na kusimamia afua za lishe na kuhakikisha Wananchi wanapata Mulo Kamili.
Miongoni mwa viashilia vya Lishe kwa ngazi ya Kata ni pamoja na Idadi ya Wanafunzi wanaokula Shuleni, Sheria ndogo za Lishe za Mitaa/Vijiji, Idadi ya Shule za Msingi/Sekondari zinazotoa huduma ya Chakula, Idadi ya Kaya zenye Wajawazito zilizotembelewa na Mhudumu wa Afya ngazi ya jamii, Idadi ya watoto chini ya miaka 5 wenye utapiamlo mkali, taarifa ya robo mwaka ya shule zinazotoa chakula, Idadi ya Vijiji/Mitaa vinavyoadhimisha siku ya lishe, pampoja na Idadi ya Vijiji/Mitaa vinavyobandika mabango yanayotoa ujumbe kuhusu lishe.
Katika kikao cha leo, wajumbe wamepata taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022-2023 ambapo maendeleo ya usimamizi sio mazuri, Vilevile wajumbe wametumia muda wa kutosha namna bora ya kutekeleza SIKU YA AFYA NA LISHE YA KIJIJI (SALIKI). Lengo kuu la SALIKI ni kuimarisha mifumo ya kijamii ya utoaji na upatikanaji wa huduma endelevu za afya na lishe ya mama, mtoto na jamii kwa ujumla.
Kwa kutambua faida nyingi za SIKU YA AFYA NA LISHE YA KIJIJI, Wajumbe kwa pamoja wameazimia kufikia tarehe 19 Machi, 2023 Kata zote za Manispaa ya Tabora ziwe zimeadhimisha siku hii muhimu kwa robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Hata hivyo katika kuhitimisha kikao hiki, Mhe. Bura amewakumbusha Watendaji Kata kusimamia miradi ya maendeleo, kusimamia vyanzo vya mapato vilivyopo chini yao, wasikilize na kutatua kero za Wananchi , lakini vilevile waimarishe upendo na watumishi wengine kwenye kata zao ili kuleta tija kwenye utekelezaji wa majukumu yao kwani upendo unawafanya wawe kitu kimoja.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.