Na Paul Kasembo-TMC.
Baraza la Ushauri Wilaya ya Tabora lajadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti 2022/2023 pamoja na mapendekezo yake yenye lengo la kuboresha na kuleta tija kwa muktadha mpana wa wananchi wa Wilaya ya Tabora.
Akifungua Mkutano wa Baraza, Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Dkt. Yahaya Nawanda, alianza kwa kuwaeleza wajumbe juu ya Mapitio ya Bajeti iliyokwisha kwa mwaka wa fedha 2020/2021kwamba kumekuwa na mafanikio makubwa sana katika utekelezaji wa maazimio ya Baraza lenyewe.
Ambapo Manispaa katika utekelezaji wa yatokanayo na Mkutano wa mwakwa wa fedha 2021/2022 imeweza kufautilia vifaa vya na fedha zilizotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya , ambapo mrejesho wake ni kwamba vifaa hivyo vilitumika kwenye ujenzi wa Ofisi za Kata.
Aidha fedha kwa ajili ya ukarabati wa Ukumbi wa Taasisi (Sanamu ya Mwl Nyerere) kiasi cha zaidi ya Tzs Mil.90 zilitemetengwa, pamoja na kufanya mchakato wa upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuweka vitega uchumi (Maduka) kuzunguuka Uwanja wa Vita unaendelea.
Akisoma taarifa ya makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Dkt. Peter Nawanda alisema kuwa, Manispaa ya Tabora imekusudia kufuata misingi itakayozingatia kufikia shabaha za ukusanyaji mapato.
Ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ushiriki wa Sekta binafsi kwenye shughuri za maendeleo, kuimarika kwa uchumi wa Taifa, kuendelea kuwa na utosherevu na upatiakanaji wa chakula ndani ya Manispaa , uwepo wa amani, usalama na utulivu miongoni mwa wananchi wa Manispaa ya Tabora.
Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Manispaa imepanga kuwa na vipaumbele vingi vyenye tija vikiwamo;
Kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa kubuni vyanzo vingine vipya 9, kujenga stendi ya kisasa katika eneo la Inala, kujenga stendi ya malori katika barabara zinazounganisha Njia kuu za Mikoani kuja stendi ya Inala.
kujenga hosteli ya wanafunzi, kujenga shopping mall mbili za kisasa zaidi, kuboresha eneo la PPP Kitete kwa ajili ya kujenga vibanda vya biashara vvyenye ghorofa, kuanzisha maegesho ya magari madogo katikati ya mji.
Sambamba na kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kutumia teknolojia ya TEHAMA, kuongeza fedha kwa ajili ya miundombinu ya Sekta za Afya, na Elimu, kuwezesha wananchi kiuchumi kwa kutoa mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Kando na hayo, pia Manispaa imejipanga kutekeleza mpango wa Bajeti yake kwa kuzingatia mikakati kama ifuatavyo; kukamilisha Miradi viporo ikiwamo jengo la Utawala , Hospitali ya Wilaya , Miundombinu ya Elimu na Afya,
Ulipaji wa fidia kwa wananchi kwa ajili ya kutatua migogoro mbalimbali na kutwaa maeneo ya uwekazaji wa viwanja, kudhibiti utoroshaji wa mazao ya kilimo na misitu kwa kuendelea kuweka vizuizi katika njia ambazo hutumika na wafanyabiashara.
Pamoja na kuingia mikataba na wakusanyaji wa mapato katika vyanzo vyote ili wawepo muda wote wa kukusanya mapato, kuhamasisha jamii kuchangia miradi ya maendeleo pamoja na kutoa elimu kwa wafanyabiashara waone umuhimu wa kulipa kodi.
“Katika hili naomba nitoe wito kwa Wadau wa Maendeleo katika Manispaa ya Tabora wakiwamo wafanyakazi, wafanyabiashara, Waheshimiwa Madiwani na Taasisi zisizo za Kiserikali waweze kushiriki kikamilifu kwenye kuchangia shughuri na utekelezaji wa Bajeti hii ili juweza kufikia malengo yaliyo tajwa”, alisema Dkt. Nyanja.
Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Tabora Mhe. Ramadhani Kapela, alimshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu kwa namna ambavyo anaendesha Nchi, na kuipatia fedha nyingi Manispaa ya Tabora ambazo zimejenga miundombinu ya Elimu na Afya.
Aidha Meya akampongeza Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi na wataalamu wa Manispaa kkwa namna ambavyo wanachapa kazi nzuri, n kwamba wana nia njema sana Manispaa ya kuivusha kuja kuwa Jiji.
Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imeomba kuidhinishiwa fedh jumla ya Shilingi 44,954,619,932.16 ambapo kati ya fedha hizo Tzs 10,626,677,093.24 ni Ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka Serikali Kuu, Tzs 25,415,574,012.00 ni fedha za Mishahara.
Aidha Tzs 5,451,254,158.25 ni fedha za Mapato ya Ndani (mapato halisi Tzs 4,781,615.100 na mapato fungwa Tzs 669,639,058.25) ambayo imeidhinishwa na Baraza la Ushauri Wilaya ya Tabora.
MWISHO
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.