HALMASHAURI ya Manispaa yaTabora inatarajia kukusanya jumla ya shilingi bilioni 43.9 zinatarajiwa katikabajeti ya mwaka wa fedha 2019/20 kutokana mbalimbali.
Taarifa hiyo imetolewa hivi karibuni na Mchumi wa Manispaa ya Tabora JosephKashushura wakati wa kikao cha Baraza laMadiwani kupitia mapendekezo ya bajeti .
Alisema katika mapato ya ndani ya Halmashauri wana lengo lakukusanya shilingi bilioni 4.6 sawa na ongezeko la asilimia 10 ukilinganisha namasikio ya mwaka 2018/19 wa bilioni 4.2 kutoka vyanzo vya ndani.
Kashushura alisema kutokaSerikali Kuu na kwa wahisani wanatarajia kupata jumla shilingi bilioni 39.2ikiwa ni pungufu ya asilimia 34 ukilinganisha na bilioni 59.8 ya mwaka 2018/19.
Alisema bajeti ya ruzukukutoka Serikali kuu na wahisani imepungua kutokana na kukamilika kwa baadhi yamiradi ya barabara ambazo zimeshajengwa kwa kiwango cha lami katika Manispaa yaTabora.
Kashushura alivitajavipaumbele katika bajeti ijayo kuwa ni uendelezaji wa jengo la utawala ambalolimetengewa milioni 200 , kuwa na fedha za fidia sehemu ambapo vitajengwaviwanda milioni 100 , uboreshaji wa miundombinu ya sekondari na shule za msingimilioni 100, mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu milioni 244.4
Aliongeza kuwa vipaumbelevingine ni shughuli za lishe zimetengewa milioni 117, mishahara ya vibarua washughuli za mazingira milioni 108.8, uendeshaji wa Hospitali milioni 80 ,kulipa madeni milioni 50 na serikali kuu kuwaletea bilioni 1.5 kwa ajili yaHospitali ya Wilaya.
Kashushura alisema kuwa kiasi cha shilingi bilioni 1zimetengwa kwa ajili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata29 za Manispaa ya Tabora na kuongeza kuwa mwaka ujao watabuni vyanzo vipyavitano vya mapato.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.