Na Paul Kasembo
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa yaTabora limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa jinsi alivyowasilishahotuba yake ya kwanza katika Mkutano wa 76 kwenye Baraza Kuu la Umoja waMataifa.
Tamko hilo limetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Mhe.Ramadhani Kapela kwa niaba ya Madiwani wenzake walipokuwa kwenye Baraza Maalumla Madiwani lililokuwa likijadili na taarifa ya hesabu kwa mwaka wa fedha2020/2021.
Alisema wao kama wawakilishi wa wananchi kutokaKata mbalimbali za Manispaa ya Tabora wameguswa na kuvutiwa na mambo mbalimbaliyaliyomo kwenye hotuba hiyo yakiwemo Tanzaniakuendeleza ushirikiano wa karibu katika siasa za kimataifa wenye lengo lakukuza uchumi na ustawi wa wananchi wa Tanzania.
Mhe.Kapela alisema jambo lingine lililowagusa katika hotuba yake ni pamoja nasuala la kuweka nguvu za pamoja katika kukabiliana na janga lamaambukizi ya virusi vya UVIKO 19.
Alisemawao kama Madiwani wataendelea kumuombea kwa Mungu ili aendelee na kazi nzurianazozifanya kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi na kuwatengenezeaWatanzania mazingira ya kuwa na afya nzuri .
AidhaMstahiki Meya aliwataka Madiwani wote kuendelea kutoa elimu kwa watu wao juu yaumuhimu wa kushiriki zoezi la kupata chanjo ya kukabiliana na jana la UVIKO 19ambazo zinaendelea kutolewa kwenye maeneo mbalimbali Manispaa ya Tabora.
Alisemakama viongozi wa Kitaifa, Mkoa na Wilaya wamechanja ni vema wananchi naowakachanja ili kulinda nguvu kazi ya Taifa isije ikapotea na kurudisha nyumauchumi wa Manispaa ya Tabora na Taifa kwa ujumla.
“Nduguzangu Waheshimiwa, watumishi wa Manispaa yetu, viongozi wa Serikali, viongoziwa dini na wadau wote mbalimbali Manispaa ya Tabora, tujitokeze kupata chanjoya UVIKO 19 ambayo kwa sasa inatolewa takribani maeneo yote ya huduma za afyahapa Manispaa, kama kiongozi wetu wa Taifa amechanja, viongozi wengine wa ngaziya kitaifa wamechanja, na kimkoa Mkuu wetu wa Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Wilayawamechanja nikiwemo mimi pia nimechanja, Mkurugenzi nae amechanja wewe mwingineunangojea nini kupata chanjo?”, Mhe. Kapela alieleza na kuuliza kwa msisitizo.
Katikahatua nyingine Barazala Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kwa kauli moja limepitishataarifa ya ufungaji wa hesabu za Halmashauri kwa mwaka 2020/21.
Wakichangia taarifa hiyo Madiwani wamewataka wataalamukufanyia kazi kasoro zote zilizojitokeza katika ukaguzi uliopita ili suala lakupata hati chafu lisijirudie tena.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawandaamewataka Madiwani kusaidia kutoa elimu kwa watoto waliopo katika Kata zaokujiepusha na vitendo vya uhalifu.
Alisema kuna baadhi ya watoto ni wanafunzi hivi karibunikatika Manispaa yetu wamekamatwa kwa tuhuma za kushiriki vitendo vya uhalifuikiwamo ukataji mapanga na kuwanyang’anya watu mali zao.
Dkt. Nawanda alisema kuwa mtoto hakumuondoi kwenye kosa kamaatabainika kushiriki vitendo vya kiharifu.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.