Baraza la Madiwani Manispaa ya Tabora imepitisha mapendekezo ya makisio ya kukusanya shilingi bilioni 50.7 katika bajeti ya mwaka wa fedha ujao wa 2021/2022.
Mpango wa Maendeleo na Bajeti yam waka 2021/2022 ambao huwasilishwa Hazina ambapo uchambuzi hufanywa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa ajili ya kupatiwa na kuangalia kama kama imezingatia vigezo (Scrutiny). Pamoja na kuzingatia Sheria ya Bajeti namba 11 ya mwaka 2015, Mpango na Bajeti yam waka 2021/2022 ambapo umeandaliwa kwa kuzingatia mabo yafuatayo:-
Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mpango wa maendeleo wa miaka mitano Awamu ya Pili kwa kipindi cha 2017/2018- 2021/2022, Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) 2030,Dira ya Taifa ya Maendeleo (National Vision 2025), Mfumo wa Fulsa na Vikwazo vya Maendeleo (O & OD), Vipaumbele vya Taifa kwa mwaka wa fedha 2021/2022, Vipaumbele vya Halmashauri ya Manispaa ya Taborana Muongozo wa Kitaifa wa Upangaji Mipango na Bajeti wa mwaka 2021/2022 ambao umetolewa kwa kuzingatia Sheria ya Bajeti namba 11 ya mwaka 2015.
Akiwasilisha bajeti hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa Ndg. Immanuel Dyelu ambaye ni kaimu Afisa Mipango wa Manispaa ya Tabora alisema makusanyo yajayo yatatokana na vyanzo mbalimbali vya mapato ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 45.6 ni ruzuku kutoka Serikali kuu na Halmashauri imelenga kukusanya shilingi bilioni 5 fedha kutoka vyanzo vyake vya mapato ya ndani. Alisema katika mwaka ujao wa fedha wamepanga kutumia shilingi bilioni 7.6 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha Dyelu alivitaja vipaumbele katika bajeti ijayo ni ujenzi wa Stendi kuu yenye eneo la ukubwa wa Hekari 50 katika Kijiji cha Inala , ujenzi wa soko la kisasa, ukarabati wa machinjio, uendelezaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, uboreshaji wa miundombinu ya elimu , soko kuu, barabara za Manispaa na ukarabati wa ukumbi wa sanamu ya Mwalimu Nyerere.
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora inafikia malengo ya kuwahudumia wananchi wake kupitia mpango wa miaka mitatu 2021/2022 – 2023/2024 kwenye Sekta ya Kilimo, Mifugo, Elimu Msingi, Elimu Sekondari, Ardhi na Maendeleoya jamii zitaonesha matokeo chanya ya malengo kaika kutekeleza mpango wa miaka mitatu.
Katika utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka 2021/2022 pamoja na majukumu mengine Halmashauri ya Manispaa ya Tabora itajikita kwenye vipaumbele vikiwamo:-
Kwa upande wake Mhe. Ramadhani Kapela ambaye ndiye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora aliipongeza sana Menejimenti na watumishi wote kwa namna ambavyo wanafanya kazi, aidhaa aliwapongeza sana Waheshimiwa Madiwani, Watendaji wa Kata na wote wanaoshiriki kwenye shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye Kata zao.
Mwisho
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.