Na Paul Kasembo-TMC.
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora itaendelea kuwanufaisha Vikundi mbalilmbali vyote vinavyokidhi vigezo vya kupata mikopo vikiwamo vya Vijana, ambapo kupitia mapato ya ndani imeweza kuwapatia Tzs Milioni 20 Kikundi cha Vijana cha Bright Vision kilichopo Mtaa wa Mihogoni Kata ya Mbugani hapa Manispaa ya Tabora.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuzindua rasmi Mashine ya Kufyatulia Tofali iliyonunuliwa na vijana hao baada ya kupata mkopo huo muwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Dr. Peter Maiga Nyanja ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Mnispaa ya Tabora Bi. Neema Gidion Kapesa aliwaeleza wana kikundi kuwa Mnaispaa ya Tabora itaendelea kuwawezesha Vikundi vyote vitakavyokidhi vigezo vya kupata mikopo kama ilivyotokea kwa kikundi cha vijana cha Bright Vision huku akisistiza kuwa Manispaa imedhamiria kuwainua kiuchumi zaidi wana Manispaa.
Manispaa ya Tabora imejipanga vema kabisa kuhakikisha kuwa vikundi vyote vyenye kukidhi vigezo vinapatiwa mikopo hiyo isiyokuwa na riba kbisa kani ndiyo maelekezo ya Serikali na kwa upande wa Manispaa tumejipanga vema kuwapatia zaidi ya Milioni 500 kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023, alisema Bi. Neema Kapesa.
Akisoma taarifa fupi ya kikundi Bw. Abdulhafidhi Daudi Manyori alisema kuwa kwa dhati kabaisa wananishukuru sana Ofisi ya Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Tabora, Idara ya Maendeleo ya Jamii, wadau wa Maendeleo wakiwamo MDH TABORA, Mhe. Diwani kwa jhudi zao katika kuwajali na kuwainua kiuchumi vijana hao kwani mkopo huo unakwenda kuwaboreshea maisha yao na pia kupunguz tatizo la nyumba duni katika eneo hilo na wakazi wopte wa Manispaa kwa ujumla kwani wataanza kutengeneza na kuuza tofali kwa bei nafuu zaidi ili kutoa huduma kwa wananchi wote.
Huu ni muendelezo wa utekelezaji wa lengo la Manispaa katika kuwainua wananchi kiuchumi unaotekelezwa kwa vitendo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Dr. Peter Miaga Nyanja katika kuyaishi maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ya kuinua jamii yote hasa wale wote walio kwenye vikundi na kuipaisha Manispaa kiuchumi na utekelzaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025.
MWISHO.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.