Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Kata ya Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoa wa Tabora kuwa, Uboreshaji wa Majaribio (PILOT) wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika kwa siku saba kwa kila kituo.
Uboreshaji wa majaribio utaanza siku ya Ijumaa tarehe 24 hadi Alhamisi tarehe 30 Novemba, 2023 katika vituo vitakavyoainishwa na Tume. Vituo hivyo vitafunguliwa kuanzia saa mbili kamili (02:00) asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili kamili (12:00) jioni.
UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA UTAHUSISHA MAMBO YAFUATAYO:-
Kuandikisha wapiga kura wapya waliotimiza umri wa Miaka 18 ambao ni raia wa Tanzania kwa mujibu wa sheria.
Kuandikisha wapiga kura ambao watakuwa wametimiza umri wa miaka 18 ifikapo uchaguzi Mkuu 2025.
Kuandikisha wale ambao wanazo sifa lakini hawakujiandikisha hapo awali.
Kuboresha taarifa za wapiga kura waliohama Kata au Majimbo yao ya Uchaguzi au ambao taarifa zao zilikosewa hapo awali Mf. Majina.
Kwa wale wapiga kura wanaotaka kuboresha taarifa binafsi na wanaohama vituo au vyote viwili kwa wakati mmoja wanaweza pia kuanzisha mchakato wa kuboresha taarifa zao kwa kwa njia ya mfumo wa mtandao ‘online’. Mfumo huu wa kuboresha taarifa za mpiga kura unapatikana katika mtandao wa Tume - www.nec.go.tz kwa kutumia kompyuta au simu janja kisha atabonyeza kiunganishi (link) iliyoandikwa Boresha Taarifa za Mpiga Kura au atatumia anuani ya ovrs.nec.go.tz itakayompeleka moja kwa moja kuanzisha mchakato huo. Katika mfumo huu, wapiga kura wanatakiwa kuingiza namba ya kitambulisho cha taifa (NIN), namba ya kadi ya mpiga kura, namba ya simu anayotumia kwa sasa na jina la kata kisha watapata ujumbe wenye namba ya utambulisho (token namber) ambayo wataenda nayo kituoni ili kukamilisha taratibu za kupata kadi ya mpiga kura.
Kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi zao au kuharibika.
Kuondoa wapiga kura waliokosa sifa za kuendelea kuwemo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Mfano waliofariki n.k.
MAMBO YA KUZINGATIA
Zoezi hili la uboreshaji wa majaribio litafanyika pia katika Kata ya Ikoma iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Rorya mkoani Mara.
Tumia haki yako ya msingi kwa kwenda kujiandikisha.
Tangazo Hili Limetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi S. L. P 358, DODOMA
Tel. +255 26 2323201 - 7. Nukushi: . +255 26 2323208. Barua Pepe: info@nec.go.tz, uchaguzi@nec.go.tz.
Tovuti: www.nec.go.tz. NEC ONLINE TV- TANZANIA,
Facebook - https://www.facebook.com/nec.tanzania.39 ,
Instagram - https://www.instagram.com/tumeyauchaguzi_tanzania/,
Twitter - https://www.twitter.com/tumeyauchaguzi_tanzania,
NEC APP - http://mobileapp.nec.go.tz,
NEC BLOG - www.blog.nec.go.tz.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.