• Lalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
TABORA MUNICIPAL COUNCIL
TABORA MUNICIPAL COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Ardhi
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • MIfugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Kata
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Uwekezaji
    • Vituo vya Utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Malalamiko
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi , Elimu na Afya
      • Kamati ya Maadili
      • Ukimwi
    • Ratiba
      • Vikao vya Halmashauri
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha

WAZIRI JAFO AKAGUA NA KURIDHISHWA NA UJENZI WA BARABARA ZA LAMI KM 21.3 TABORA MANISPAA

Posted on: June 6th, 2020

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemeni Jafo (MB) ametembelea na kukagua ujenzi wa barabara za Lami zenye urefu wa KM 21.3

Katika ziara hiyo Mhe Waziri alikuwa ameongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya TARURA TANZANIA, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri, Mbunge wa Tabora Mjini Mhe Adamson Mwakasaka, Viongozi mbali mbali wa Manispaa ya Tabora ambapo walitembelea na kukagua ujenzi wa mtandao wa barabara kwa kiwango cha Lami na kuridhishwa kwa namna ambavyo ujenzi huo ulivyofanyika na viwango vyake.

''Nimekuwa ziarani kwa siku sita sasa, nimetembelea na kukagua miradi yote ambayo ipo chini ya Wizara yangu ya TAMISEMI kwa mikoa saba ikiwemo na Tabora kwenye Manispaa yenu ya Tabora ambapo nimekagua na kuridhishwa sana na mradi huu wa ujenzi wa barabara KM 21.3 kwa kiwango cha Lami, huu ni moja ya mradi uliotumia fedha nyingi sana chini ya Mradi wa Kimkakati wa Uimarishaji Halmashauri za Miji na Manispaa (ULGSP) hakika nimeridhishwa HONGERENI SANA MANISPAA YA TABORA,'' alisema Mhe Jafo.

Waziri Jafo alisema kuwa yote hayo ni matokeo na matunda ya kazi kubwa inayofanywa na Mhe John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Tanzania kwa wananchi wake, na kwamba hawakukosea kumchagua Mhe Rais, kwa msingi huo kuna kila sababu ya kumshukuru Mhe Rais wetu.

Aidha katika hatua nyingine Mhe Jafo aliwaambia wananchi wa Manispaa ya Tabora waliokuwa wakimsikiliza kwenye mkutano huo wa hadhara kwamba, kupitia Mbunge wa Tabora Mjini Mhe Mwakasaka na baadhi ya Waheshimiwa Madiwani walienda kumfuata Ofisini kwake Dodoma na kumuomba fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambapo aliwaahidi kuwapatia kiasi cha Shilingi Bilioni Moja.

Kwa upande wa Elimu, Mhe Jafo aliwaeleza wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ilitoa kiasi cha Bilioni 89 kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe Nchi nzima zikiwemo na shule za Tabora Wavulana, Milambo Wavulana na Kazima Sekondari zote hizi zipo hapa Tabora Manispaa.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa ULGSP, Meneja wa TARURA Tabora Manispaa Mhandisi Edwin Kabwoto alimueleza kuwa Mradi huo wa Ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami nene umejengwa kwa awamu tatu tofauti (Three phases).

Ambapo awamu ya kwanza (LOT 1 sawa KM 6.1 ujenzi) ulifanyika chini ya ya Mkandarasi M/S SALUM MOTORS TRANSPORT Co LTD na ANAM ROAD WORKS Co Ltd, awamu yapili (LOT 2  sawa na KM 9.23) Mkandarasi alikuwa M/S SALUM MOTORS Co LTD na ANAM ROAD WORKS Co Ltd na awamu ya tatu (LOT 3 sawa na KM 6.02) Mkandarasi alikuwa ni CHONQING International Construction Corporation (CICO) na hivyo kukamilisha ujenzi wa barabara yenye urefu wa KM 21.3

 Kukamilika kwa mradi huu katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kumeongeza tija katika uzalishaji, usafirishaji wa bidhaa na abiria kutoka eneo moja kwenda lingine pia umesaidia kuboresha muonekano wa Mji na kuongezeka kwa thamani ya maeneo yaliyokaribu na barabara hizo.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA (PSLE) 2020 November 21, 2020
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 MANISPAA YA TABORA December 18, 2020
  • Usafi wa Mazingira kwa Wananchi Wote, Jumamosi ya mwisho kila Mwezi March 23, 2017
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DC KOMANYA AZINDUA SHUGHURI ZA UHAMASISHAJI WA BIMA YA AFYA YA JAMII (CHF ILIYOBORESHWA) MANISPAA YA TABORA

    January 19, 2021
  • MPANGO WA TAIFA WA KUDHIBITI KIFUA KIKUU NA UKOMA WADHAMIRIA KUZIFIKIA KATA ZOTE TABORA MANISPAA

    December 18, 2020
  • MSTAHIKI MEYA TABORA MANISPAA AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA VILEO

    December 17, 2020
  • RC AONGOZA WAKAZI WA KIJIJI CHA IGOMBE MANISPAA YA TABORA KUADHIMISHA MIAKA 59 YA UHURU KWA KUPANDA MITI ZAIDI YA 300

    December 09, 2020
  • Angalia Zote

Video

Ziara ya Waziri Jafo Shule ya Msingi Ipuli
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Capital Investment Plan
  • Tabora Master Plan 2015 - 2035
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA
  • Taarifa Mbalimbali
  • Fomu ya maombi ya Leseni
  • Jarida 2020
  • Taarifa kwa Umma
  • Fursa za Uwekezaji

Kurasa Zinazofanana

  • IKULU
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mkoa wa Tabora

Waliotembelea Tovuti

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Manispaa Tabora - Barabara ya Boma

    Anwani ya Posta: S.L.P 174 Tabora

    Simu ya Ofisi: 026-2604315/6088

    Simu ya Mkononi: 0786820518

    Barua Pepe: md@taboramc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.