Na Paul Kasembo;
Vijana wametakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo katika Mkoa wa Tabora kwa kuwa mawazo yenye kutoa muelekeo wa ufumbuzi na baadaye kutaguta Mitaji kutoka Halmashauri zao na Taasisi za Kifedha zilizopo katika Halmashauri zao.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 18 Desemba, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi. Dkt. Batilda Burian wakati akifungua Kampeni kwa Vijana wa Mkoa wa Tabora ijulikanayo KIJANA ONGEA NA MAMA iliyofanyika katika Ukumbi wa Mwanakiyungi uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Tabora.
Akiongea wakati wa ufunguzi, Mhe. Batilda alisema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pesa nyingi sana na kuwekeza katika ujenzi wa Vyuo vya Veta ambapo Mikoa mingi imejenga na kutoa fursa kwa vijana kukuza talanta zao ili wazitumie kujiajiri na kuajiri wenzao ambapo kwa Mkoa wa Tabora ilipokea zaidi ya Tzs Bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa Vyio vya Veta.
Kwa upande wa Uwekezaji Mkoa wa Tabora kwa sasa unao mradi mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa awamu ya Tatu (SGR) Makutopora - Tabora ambapo mpaka sasa wazawa 770 kati ya 1,142 wamepata ajira katika mradi huo.
Pamoja na mambo mengine, Mhe. Batilda Wakuu wa Wilaya wote kwenda kuanzisha Kiwanda kimoja kwenye Wilaya zao, kiwanda ambacho kitatoka na rasilimali/bidhaa watakazo chagua wao wenyewe vijana na hivyo kutoa ajira kwao.
"Nitumie fursa hii kuwaagiza Wakuu wa Wilaya wote kwenda kuanzisha na kusimamia Kiwanda kimoja kitakachotokana na bidhaa au rasilimali zao vijana wenyewe na kiwe chanzo cha ajira kwa vijana, na kujiajili wenyewe na ndiyo maana tumewaita hapa Wakuu wa Wilaya wote," akisema Mhe. Batilda.
Aidha amewataka vijana kutembelea abustani za Wanyama kama vile Tabora Zoo ili waweze kuona fursa zilizopo pale zikiwamo uuzaji wa vinywaji, chakula nk.
Kwa upande wao vijana walimpongeza na kumshukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi. Dkt. Batilda Burian kwa kuamua kuyatekeleza maelekezo ya Mhe. Rais kwa vitendo, kwani kwa kufanya hivyo kutawawezesha vijana kufunguka changamoto zao na Serikali kusaidia upatikanaji wa ufumbuzi na hivyo kuleta mafanikio katika Uchumi wao.
Mkuu wa Mkoa waTabora amekuwa mstari wa mbele kahisa katika kuhakikisha kuwa Mkoa unapiga hatua kimaendeleo kupitia rasilimali watu, rasilimali vitu kwa kutumia fursa zilizopo hapa Mkoa wa Tabora.
MWISHO.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.