Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Yahaya Esmail Nawanda wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Masagala, Kata ya Misha ambapo yeye Mkuu wa Wilaya ndiye alikuwa Mgeni rasmi.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Dkt. Nawanda aliwaeleza mamia ya wananchi waliokuwa wamefurika katika viwanja hivyo kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan haipo tayari kuona watoto wakinyanyasika, kudharirika, wala kupata ukatili wowote wa kijinsia na kwenye Wilaya anayo iongioza yeye Dkt. Nawanda hatakubali kabisa kutokea kwa mambo hayo.
“Niwahahakishie wananchi wangu wa Wailaya ya Tabora kuwa, watoto wote waliomo kwenye Wilaya hii ninayo iongoza mimi sipo tayari kabisa kuona wakipatwa na matatizo yoyote ya kijinsia, unyanyasaji wala aina yoyote ya ukatili kwakuwa nimepewa dhamana ya kuwalinda katika Wilaya hii”, alisema Dkt. Nawanda.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Mhe. Ramadhani Shabani Kapela (Diwani) alimueleza mgeni rasmi pamoja na wananchi kuwa, sheria ya mtoto inamtafsiri kama mtu mwenye umri wa chini ya miaka 18. Hivyo watoto ni sehemu ya jamii na ndiyo tegemeo endelevu la Taifa lolote, ni wajibu kwa wazazi kuwalea vizuri na kuwaendeleza, wasiachie Serikali peke yake katika hili na wazazi au walezi wawajibike.
Naye Diwani wa Kata ya Misha Mhe. Yassin Kushoka alimshukuru sana Mkuu wa Wilaya kwa kuitikia ombi la kwenda kwenda kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, japokuwa anazo kazi nyingi lakini Mkuu wa Wilaya amekubaliana na kuhudhuria.
Kwa upande wao watoto walisema kuwa, pamoja na sharia ya mtoto kubainisha bayana haki za mtoto bado na wao watoto wanakutana na changamoto za kupata haki zao kama vile kuapata chakula kwa wakati, kutohudhuria masomo, malazi duni na kufanyiwa ukatili wa kingono, kimwili na kisaikolojia.
Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kila mwaka ya tarehe 16, Juni kukumbuka mauaji ya halaiki ya watoto yaliyofanywa na majeshi ya Makaburu katika kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini mwaka 1974.
Watoto hao waliuawa kikatili wakiwa katika maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi kama vile kutumika kwa lugha ya ki-Afrika na kuwafundishia watoto wa ki-Afrika tu ili hali watoto wa kizungu wakitumia lugha ya kiingereza.
Siku hii ilianza rasmi kuadhimishwa baada ya Umoja wa Mataifa kuridhia kupitisha Mkataba wa Kulinda Haki za Mtoto mnamo mwaka 1990.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.