Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Burian amezindua rasmi ki- Mkoa utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi hafla ambayo imefanyika katika Mtaa wa Milambo, Kata ya Ngambo Halmasahuri ya Manispaa ya Tabora.Akihutubia wananchi ambao walijitokeza kwenye hafla hiyio, Dkt. Batilda aliwaeleza kuwa ujio wa zoezi hilo la Anwani za Makazi ni muhimu sana na limekuja kwa wakati muafaka, kwani baada ya zoezi hilo kutafuatiwa na zoezi la SENSA.Dkt. Batilda aliwataka wananchi kujitokeza kwenye utekelezaji wa Mfumo huo huku akiwasihi kutoa ushirikiano mkubwa zaidi kwa timu itakayokuwa inawafikia majumbani mwao ili kuweza kufanisha jambo hilo kwa ufanisi zaidi.Niwaombe wananchin wote Tabora kushiriki kikamilifu kwenye kazi hii inayokwenda kuanza hivi karibuni, mkatoe ushirikiano mkubwa kwa wataalamu wetu watakao wafikia kwenye utekelezaji ili sisi kama Mkoa tuweze kufanya vizuri, kwa wakati na kwa ufanisi zaidi na kwa wakati uliopangwa, alisema Dtk. Batilda.Aidha alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Dkt. Yahaya Nawanda kwa kuweza kuanza utekelezaji huo na kuwa kinara kulinganisha na Wilaya nyingine, ambapo kwa Wilaya ya Tabora pekee ndiyo wamefikia asilimia 40, kulinganisha na Wilaya nyingine ambazo hazijafikia zaidi ya asilimia 20. Awali Mkuu wa Wilaya ya Tabora akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mhe. Dkt. Yahaya Nawanda alimshukuru sana Mhe. Samia suluhu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuliona hilo na kuamua litekelezwe ili kwenenda na dunia ya sasa. Aidha akamshukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Burian kwa kuamua kuichagua Wilya ya Tabora kuwa sehemu ya uzinduzi wa utekelezaji wa kazi hiyo, huku akimuahidi kuwa Wailya ya Tabora itafanya vizuri sana kwenye utekelezaji huo na kwamba litakuwa la usahihi, kwa wakati na kwa ufanisi zaidi kwakuwa viongozi wote walishirikishwa kikamilifu kwenye semina elekezi juu ya kazi hiyo.Nikuahidi Mkuu wa Mkoa kuwa sisi Wilaya tumejipanga vema sana kwenda kutekeleza kazi hii, na kwamba tuna uzalendo, nguvu n uelewa mkubwa wa jambo hili na nikuahidi tuu kuwa sisi tutakuwa wa kwanza kutekeleza kimkoa na tutafanya vizuri sana, alisema Dkt. Nawanda.Hafla ya Uzinduzi ilihudhuriwa pia na baadhi ya viongozi mbalimbali akiwepo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ta Tabora Ndg Mohamed Katete, Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini Mhe. Adamson Mwakasaka, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Mhe. Ramadhani Kapela, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Ndg Seif Salum.Kukamilika kwa utekelezaji buu wa Anwani za Makazi na Postikodi kutaiwezesha jamii yote kuwa na mawasiliano ya uhakika, upatikanaji wa huduma bora zaidi za kijamii na uhakika wa kuwafikia
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.