Na Alex Siriyako:
Miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imengara katika mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 baada ya miradi yote saba yenye thamani ya zaidi ya bilioni kumi na nane kubata baraka za Viongozi Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa wakiongozwa na Ndugu Godfrey Eliakim Mnzava.
Mwenge wa Uhuru leo Agosti 20, 2024 umekimbizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ambapo miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na Madarasa matano na vyoo yaliyopo Shule ya Sekondari Itonjanda, Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) katika Hospitali ya Saint Anna,s Mission, Kituo cha Mafuta ”SIZYA PETROL STATION”, Mtandao wa barabara za rami wenye urefu wa kilometa10.7, Mradi wa maji Manispaa ya Tabora unaonufaisha vijiji vya Ntalikwa, Tumbi, Kakola pamoja na Magoweko, Bustani ya Miti , pamoja Mradi wa Usafirishaji Bodaboda (Kikundi cha Ujamaa).
Aidha Ndugu Godfrey Eliakim Mnzava, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa katika miradi yote hii amezindua madarasa hayo matano na Vyoo katika Shule ya Sekondari Itonjanda, amezindua mradi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje ( OPD) katika Hospitali ya Saint Anna,s Mission, amezindua kituo cha mafuta SIZYA PETRO STATION, ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mtandao wa barabara za rami zenye urefu wa kilometa 10.7, amezindua mradi wa maji Tabora , amezindua bustani ya miti , lakini pia ametembelea na kukagua mradi wa bodaboda wa kikundi cha Ujamaa.
Vilevile Viongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru wamesisitiza sana katika jumbe zao, Jamii kuendelea kuchukua tahadhari na kupambana na maradhi kama UKIMWI, Malaria, Dawa za kulevya, pamoja na Kutunza Mazingira.
Kwa msisitizo sana, Ndugu Godfrey Mnzava ameissitiza Jamii ya Tabora kuepuka sana vitendo vyote vya vyenye viashiria vya Rushwa hasa katika kipindi hiki ambacho Nchi inaelekea kwenye chaguzi, na katika hili amewaasa Jamii ya Tabora ikashiriki vyema sana kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa, kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyojieleza.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Manispaa Tabora, 4 Barabara ya Kiwanja cha Ndege
Anwani ya Posta: S.L.P 174, 45182 Tabora
Simu ya Ofisi: +255 262606088
Simu ya Mkononi: +255
Barua Pepe: md@taboramc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.