Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imepongezwa sana kwa kupata Hati Safi ya Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021. Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Balozi Batilda Buriani ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano Maalumu wa Kujadili taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Tabora.
Akizungumza wakati wa majadiliano hayo Mhe. Batilda alisema kuwa imekuwa ni faraja kubwa sana kwake yeye mwenyewe, Serikali ya Mkoa, Manispaa ya Tabora na kwa wananchi wote kwakuwa kupata Hati safi kunaifanya Manispaa kupata fedha Zaidi kutoka Serikali kuu kwa ajili ya mambo mbalimbali ikiwamo fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo nk.
“Niwapongeze sana Manispaa ya Tabora, Baraza la Madiwani, Menejimenti na watumishi wote wa Manispaa bila kusahau wadau wote kwa kuwezesha kupatiakana kwa hati safi baada ya ukaguzi wa fedha kwa mwaka 2020/2021, mmeiheshimisha sana Manispaa ya Tabora”, alisema Mhe. Batilda.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Mhe. Ramadhani Shabani Kapela alimshukuru sana Mungu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuikumbuka Manispaa ya Tabora hata ameipatia fedha nyingi kwa ajili utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kisha akamshukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Balozi Batilda Buriani kwa namna ambavyo amekuwa akiisaidia Manispaa ya Tabora katika kutekeleza shughuri zake za kila siku akisaidiwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Dkt. Yahaya Esmail Nawanda ambaye amekuwa na msaada mkubwa sana tangua wasili Wilaya aya Tabora na hata sasa Manispaa imepata hati safi.
“Kwa dhati ya moyo wangu kabisa na kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Tabora, Mkurugenzi na Menejimenti yake tunawashuruni nyote kwa kuwezesha Manispaa yetu kupata hati safi, ni jamboa mbalo lie]likuwa limekwama kwa muda wa miaka kadhaa kuipata hati safi, tunawashukuru san asana, juhudi zenu zimeleta mafanikio haya”, alisema Mstahiki Meya Kapela.
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 ilifanyiwa ukaguzi wa hesabu za Serikali katika kipindi cha Oktoba 2021.
Katika kipindi hicho Halmashauri ilipata hoja 42 (hoja 35 za kitabu kikubwa na hoja 6 za miradi ya Mradi ya Afya) na hoja 49 (44 za kitabu kikubwa na hoja 5 za Mradi wa Afya) za kipindi cha miaka ya nyuma (2012/2013 hadi 2019/2022)
Baada ya zoezi la uhakiki wa majibu ya hoja Halmashauri kwa kipindi cha mwaka 20202/2021 imebakiwa na hoja 21 za sasa na hoja 25 za miaka ya nyuma.
Hivyo Menejimenti inaendelea kuzifanyia kazi hoja 21 za sasa na 25 za nyuma ili kuhakikisha kwamba zinahakikiwa na kufungwa. Na kwamba Menejimenti imefanikiwa kupunguza hoja 42 za mwaka 2022/2021 hadi hoja 21 na kupunguza hoja 49 za miaka ya nyuma (2012/2013 hadi 2019/2020) hadi hoja 25 kutokana na kuunda Kamati Maalumu ya kushughulikia hoja za ukaguzi kwa kuzingatia maelekezo ya OR-TAMISEMI.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.