Na Alex Siriyako:
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora ikiongozwa na Mwenyekiti cha chama hicho Ndugu Said Nkumba, imeridhika na ubora wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Manispaa ya Tabora.
Kamati hii inafanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Tabora, ambapo leo Agosti 11,2024 Kamati hii imekagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Tabora, ambapo miradi iliyopo chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora pamoja na Wakala wa Barabara Mkoa wa Tabora imetembelewa na kukaguliwa.
Kwa upande wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na Ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike wenye mahitaji maalumu katika shule ya sekondari Kazima pamoja na ujenzi wa jengo jipya la Utawala la Manispaa ya Tabora, miradi yote hii ipo kwenye hatua ya umaliziaji.
Kwa upande wa Wakala wa Barabara Tanzania ( TANROADS) Mkoa wa Tabora , mradi wa upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Mkoa wa Tabora umetembelewa na kukaguliwa, upanuzi huu unahusisha ujenzi wa jengo jipya la kisasa la abiria, uzio pamoja na maegesho ya magari. Kwa ujumla wake utekelezaji wa mradi huu unaendelea vizuri.
Kwa niaba ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Tabora, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Ndugu Said Nkumba amemshukuru sana Mwenyekiti wa CCM Taifa, ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuupatia Mkoa wa Tabora fedha nyingi sana za miradi ya maendeleo kwa takribani kila sekta.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Manispaa Tabora, 4 Barabara ya Kiwanja cha Ndege
Anwani ya Posta: S.L.P 174, 45182 Tabora
Simu ya Ofisi: +255 262606088
Simu ya Mkononi: +255
Barua Pepe: md@taboramc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.