Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Bw. Elias Mahwago Kayandabila pamoja na Timu ya Menejimenti watembelea Hifadhi ya Ngorongoro- Arusha Leo Mei 26, 2024. Akizungumza wakati wa kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro, Mkurugenzi alisema “Sisi kama viongozi wa serikali tumekuja hapa kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais za kuitangaza Tanzania yetu pia tutatumia fursa hizi kutangaza kazi za Mhe. Rais”.
Aidha, katika matembezi haya na wakitumia kauli mbiu ya “Royal Tour, Boresha Utalii Manispaa ya Tabora” Bw. Elias Mahwago Kayandabila alisema “Utalii huu utawezesha timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kujifunza mbinu mbalimbali za kuboresha utalii”
KARIBU UTALII HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Manispaa Tabora, 4 Barabara ya Kiwanja cha Ndege
Anwani ya Posta: S.L.P 174, 45182 Tabora
Simu ya Ofisi: +255 262606088
Simu ya Mkononi: +255
Barua Pepe: md@taboramc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.