Naibu Katibu Mkuu (Elimu) Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde amewataka Maafisa Elimu Miko ana Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri kusimamia miradi ya elimu kukamilika kwa wakati ili kuepuka kwa hoja za ukaguzi katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Hayo yameelezwa leo tarehe 15 Agosti, 2022 Mkoani Tabora wakati akifungua kikao kazi cha Mafunzo na kujengewa uwezo kwa maafisa hao kuhusu Usalama wa Mazingira na Jamii katika kutekeleza mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (Tanzania Secondary Education Quality Improvement Project – SEQUIP) katika maeneo yao ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza katika utekelezaji wake.
Dkt. Msonde aliendelea kufafanua kuwa, Serikali imeendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya elimu na fedha za mradi wa SEQUIP na kuboresha elimu ya Sekondari, kuongeza fursa ya upatikanaji wa elimu, kupunguza vikwazo vinavyosababisha wanafunzi kuacha shule, kuwasaidia wanafunzi kumaliza elimu bora ya sekondari na kupunguza changamotoza upatikanaji wa elimu nchini.
Dkt. Msonde amewataka maafisa hao katika kusimamia ujenzi wa shule hizo kuepuka migogoro ya ardhi inayoweza kutokea na kusababisha matatizo kwa kutoendelea kwa ujenzi. Aidha vilevile kusimamia ujenzi ili uendane na thamani ya fedha iliyotolewa , pia pia kusimamia utekelezaji wa ujenzi unaoweza kuzingatia muda uliowekwa ili ukamilike kwa wakati na shule hizo I;I ziweze kukamilika na wanafunzi kwa haraka.
“Ninyi ni wabobezi katika usimamizi na utekelezaji wa elimu tushirikiane sote ili miradi hii iwe yenye kuleta tija katika Taifa letu,” alisema Dkt. Msonde.
Awali akitoa maelezo mafupi Mkurugenzi Msaidizi Idara Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bi Hadija Mcheka amemuelezaNaibu Katibu Mkuu Dkt. Charles Msonde kuwa , kikao hicho kitakuwa cha siku mbili kwa kujengewa uwezo kwa maafisa hao kwa kufundishwa mada mbalimbali kutoka kwa wataalamu ili kupata ufahamu taratibu za usimamizi wa mradi na kupata nafasi ya kutoa maoni katika kufanikisha mradi unatekelezwa kwa ufanisi zaidi.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Bw. Juma Kaponda akiongea kwa iaba ya watendaji hao ameishukuru sana Serikali kwa kuendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya elimu na kuahidi kusimamia kwa kutekeleza na kufuata sheria, miongozo na taratibu zinazowataka kwa kuhakikisha Sekta ya elimu inakuwa na manufaa kwa Taifa.
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.